Treni ya SGR ina faida kiuchumi, kijamii - RC Senyamule

NA SAIDA ISSA, DODOMA MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (pichani), amesema usafiri wa treni ya kisasa una faida nyingi za kiuchumi na kijamii kwani utapunguza muda wa safari kutoka saa nane hadi tisa kwa usafiri wa mabasi hadi saa tatu na nusu kwa safari ya Dodoma – Dar es salam. Hayo ameyaeleza Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa rasmi wa safari za treni ya kisasa kwenda Morogoro – Dar es salaam kutokea Dodoma utakaofanyika Agosti 1, 2024 katika stendi kuu reli jijini Dodoma. Senyamule amesema kuwa treni hiyo ya umeme itawawezesha wafanyabiashara kusafiri kutoka mkoa mmoja wa Dar es Salaam au Dodoma na kurudi kuendelea na biashara zao ndani ya muda mfupi. "Kituo hiki cha treni kina sehemu mbali mbali ikiwemo sehemu zakufanyia biashara makundi, waje wafanyabiashara wanaotaka kufanyia biashara zao hapa, majengo ni ya kisasa, waje wawekeze kwani mkoa wa Dodoma ni mkoa wenye utalii, wageni watakao kuja na treni watajifunza na k...