Jaji Mstaafu Luanda amrithi Jaji Mlay MCT
NA MWANDISHI MAALUM MKUTANO Mkuu wa 26 wa wanachama wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), umemchagua Jaji Mstaafu Bernad Luanda (pichani) kuwa R ais wa baraza hilo kuziba nafasi iliyoachwa na jaji mstaafu Juxon Mlay, aliyefariki dunia mapema mwaka huu. Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Ernest Sungura, amewashukuru wanachama walioshiriki mkutano huo na kueleza kuwa baraza limejipanga kuimarisha huduma zake kwa wananchama ikiwemo kuwanoa waandishi wa habari. Amesema, kuanzia mwaka ujao MCT itakua inatekeleza mradi mkubwa utakaojulikana kwa jina la ‘WAJIBIKA’ ambao utakuwa wa miaka saba ambapo utakuwa na thamani ya pauni milioni 30, utakaogusa kila eneo, ikiwemo kuwajengea uwezo hata waandishi wa habari mmoja mmoja, kupiti vyombo vyao. Alieleza kuwa, jingine ambalo litafanyika mwakani, ni sherehe kubwa na za aina yake, ya mafanikio ya ‘MCT’ kwa miaka 30, tokea lilipoanzishwa mwaka 1995. Katibu Mtendaji huyo, aliwataka wanachama wenye madeni, ambay...