UVCCM yalaani wanaochochea uvunjifu wa amani
NA SAIDA ISSA, DODOMA
BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) taifa
limelaani vikali tabia ya baadhi ya watu, taasisi na jumuiya za kimataifa zenye
tabia ya kutumia vijana kuharibu na kubeza amani, umoja na mshikamano wa taifa.
Kauli hiyo ilitolewa jijini
Dodoma na Mwenyekiti wa umoja huo Mohamed Ali Mohamed ‘Kawaida’ alipokuwa
akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kikao cha kawaida cha baraza kuu la
umoja huo lililokutana hivi karibuni.
"UVCCM tunalaani vikali
vitengo viovu vinavyowatumia vijana ama kuwahusisha katika matukio hayo na hatutafumbia
macho matukio hayo", alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha aliongeza kuwa Baraza hilo
linawataka vijana wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la uchaguzi
wa serikali za mitaa kwa kujiandikisha katika daftari la mkazi,kugombea na
kupiga kura na kwamba UVCCM itawaunga mkono.
"Baraza kuu la umoja wa
vijana wa Chama cha Mapinduzi kwa kauli moja tunazipongeza Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa namna zinavyoendelea
kuwatumikia wananchi kwa vitendo kupitia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama
cha Mapinduzi yam waka 2020 - 2025", alisema.
Comments
Post a Comment