'Zanzibar Matibabu Card' yashinda tuzo ya WSIS

NA MWANDISHI MAALUM, USWISI WIZARA ya Afya Zanzibar imetunukiwa tuzo ya kimataifa ya ‘ World Summit on the Information Society’ (WSIS) kutokana na mafanikio ya utekelezaji wa mfumo wa matibabu kwa njia ya kadi maalum ya kidijitali ijulikanayo kama ‘ Zanzibar Matibabu Card’ , ambao umewezesha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi kupitia teknolojia. Hafla ya kukabidhi tuzo hiyo ilifanyika Geneva, Uswisi na kuhudhuriwa na Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania, Jerry Slaa, Balozi wa Tanzania Geneva, Abdallah Possi, pamoja na wajumbe kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar (e-GAZ) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, alisema mpango huo ni uthibitisho wa dhamira ya taifa kutumia teknolojia kuboresha maisha ya wananchi. Alieleza kuwa mfumo huo umeunganisha vituo vyote vya afya vya umma na taarifa za m...