Wafikieni watumishi wa ngazi za juu, viongozi waandamizi – Mhandisi Zena
NA MWANAJUMA SAID, IPA KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, amelitaka Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar (IPA) kuwafikia watumishi wa kada za juu na viongozi waandamizi ili kuongeza ufanisi katika usimamizi na utoaji wa huduma za umma. Akizungumza wakati wa mahafali ya 18 ya chuo hicho huko Tunguu, alisema kuwa kwa muda mrefu IPA inatoa mafunzo ya muda mfupi yanayolenga zaidi watumishi wa kada za chini na kati, wakati kundi la viongozi wa ngazi za juu likibaki nyuma kupata mafunzo maalum yanayohitajika katika nafasi zao pekee. “Kuna haja sasa kuelekeza nguvu za kuwafikia watumishi wa kada za juu na viongozi. Ni muhimu viongozi wa ngazi zote wafikiwe kulingana na mahitaji yao ya mafunzo na upatikanaji wao”, alisema Mhandisi Zena. Alisema kuimarika kwa mafunzo hayo kutachochea maboresho ya mifumo ya uongozi, kuongeza uwajibikaji na kuleta matokeo chanya kwa wananchi katika taasisi za umma. KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiong...