Posts

Showing posts from July, 2026

Hemed azindua programu ya malezi, makuzi ya awali ya mtoto

Image
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imezindua Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto pamoja na Kituo cha Kulelea Watoto katika Soko la Mwanakwerekwe, ikiwa ni hatua ya kuimarisha ustawi wa watoto na kuwawezesha wazazi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji. Akizindua programu hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi , Makamu wa Pili wa Rais, Hemed Suleiman Abdulla , alisema Serikali inaamini kuwa uwekezaji katika malezi na makuzi ya awali ya mtoto ni msingi wa kujenga taifa lenye afya, elimu bora na uchumi imara. Alisema programu hiyo itawaunganisha wazazi na walezi katika kupata huduma muhimu zinazohusu afya, lishe, ulinzi na maendeleo ya watoto tangu wakiwa wadogo. Hemed alisema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya malezi kwa kuanzisha vituo vya kulelea watoto katika masoko, hospitali na skuli za awali ili kuwawezesha wazazi kutekeleza majukumu yao bila kuwa na hofu kuhusu usalam...