
Waandishi wahimizwa kuepusha migogoro NA ASYA HASSAN WAANDISHI wa habari wametakiwa kujikita katika uandishi wa habari zenye mnasaba wa kuleta amani katika jamii kwa lengo la kuepusha migogoro inayoweza kusababisha vuruga ndani ya jamii. Hayo yalisemwa na Meneja Mkaazi wa shirika la Search for Common Ground, Hussein Sengu, alipokwa katika mafunzo ya usuluhishi na ujenzi wa amani yaliyowashirikisha waandishi wa habari kupitia mradi wa dumisha amani unaosimamiwa na shirika hilo. Aliseama waandishi wa habari ni watu watakao weza kuifanya jamii kuwa na Amani ama kuisababisha kuingia matatani hivyo ni vyema kuzitumia kalamu na midomo yao kwa uweledi na ufanisi ili kuona Amani iliyopo inazidi kuimarika. Meneja huyo alisema lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya namna ya kuripoti habari zenye mlengo wa kuleta amani katika jamii na sio kuongeza tofauti ziliyopo ndani ya maeneo yao. Sambamba na hayo alisema jamii imekuwa ikikabiliwa na matatizo tof...