Simbaya Mkurugenzi mpya UTPC

MUUNGANO wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umepata Mkurugenzi Mtendaji mpya kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Mkurugenzi wake, Aboubakar Karsan.


Taarifa iliyotolewa na Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo (katikati pichani) kupitia mtandao wake wa Twitter imemtaja Mkurugenzi huyo kuwa ni Keneth Simbaya ambaye aliwahi kuiongoza taasisi hiyo siku za nyuma.

“Nikiwa Rais wa UTPC nina furaha kutangaza kuwa Union of Tanzania Press Clubs, (Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania) UTPC, imepata Mkurugenzi Mtendaji mpya Ndg. Kenneth Simbaya (kulia kwangu), amechukua nafasi ya Abubakar Karsan (kushoto kwangu) ambaye amestaafu,” alieleza Nsokolo katika taarifa yake hiyo iliyoambatana na picha akiwa na watendaji wawili hao.

Kwa niaba ya uongozi na wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), inampongeza Ndg. Simbaya kwa kuaminiwa na bodi ya wakurugenzi ya UTPC kushika wadhifa huo lakini pia Ndg. Karsan kwa utumishi wake uliotukuka kwa taasisi hiyo inayowaunganisha wanahabari wa Tanzania kwa lengo la kuimarisha weledi na ustawi wa tasnia ya Habari nchini.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango