TIB yaanika sababu za kuweka riba nafuu mikopo ya kilimo

NA MWANDISHI WETU, MWANZA BENKI ya Maendeleo Tanzania (TIB) imepongezwa kwa kutoza riba nafuu kwa wakulima na wawekezaji wanaojishughuisha na za uzalishaji, usindikaji mazao na masoko hasa kwa wakopaji wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo hapa nchini. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Chande (pichani kushoto), wakati alipotembelea banda la benki ya TIB, kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyokua yakifanyika katika viwanja vya Rock City Mall, jijini Mwanza. Chande alionesha kufurahishwa na huduma za mikopo inayotolewa na benki hiyo kupitia dirisha la kilimo linalowalenga wakulima na wawekezaji wenye miradi ya kilimo na ufugaji. Akiwa bada la benki hiyo, Chande alijulishwa kuwa riba inayotozwa kupitia kwa mikopo hiyo ni asilimia tano kwa mwaka kwa wakopaji wa moja kwa moja toka benki na asilimia 4 kwa upande wa taasisi zinazokopa kwa ajili ya kukopesha ambapo hutat...