TIB yaanika sababu za kuweka riba nafuu mikopo ya kilimo
NA MWANDISHI WETU, MWANZA
BENKI ya Maendeleo Tanzania (TIB) imepongezwa kwa kutoza riba nafuu kwa wakulima na wawekezaji wanaojishughuisha na za uzalishaji, usindikaji mazao na masoko hasa kwa wakopaji wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo hapa nchini.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Chande (pichani kushoto), wakati
alipotembelea banda la benki ya TIB, kwenye maonesho ya Wiki ya
Huduma za Fedha Kitaifa yaliyokua yakifanyika katika viwanja vya Rock City Mall,
jijini Mwanza.
Chande alionesha kufurahishwa na huduma za mikopo inayotolewa na
benki hiyo kupitia dirisha la kilimo linalowalenga wakulima na wawekezaji wenye
miradi ya kilimo na ufugaji.
Akiwa bada la benki hiyo, Chande alijulishwa kuwa riba inayotozwa
kupitia kwa mikopo hiyo ni asilimia tano kwa mwaka kwa wakopaji wa moja kwa
moja toka benki na asilimia 4 kwa upande wa taasisi zinazokopa kwa ajili ya
kukopesha ambapo hutatakiwa kukopesha kwa asilimia isiyozidi asilimia nane kwa
wateja wao.
Alisema serikali inafarijika kuona TIB inaendelea kuwahudumia wakulima
wadogo wadog, wa kati na wakubwa wanaoendesha kilimo cha kibiashara kupitia
makampuni ili kuongeza thamani shughuli za kilimo hapa nchini.
Kwa mujibu wa Afisa Biashara Mwandimizi wa Benki ya Maendeleo (TIB), John
Mboje, TIB imekua ikitoa mikopo kupitia Dirisha la Kilimo ambayo kipindi
cha marejesho ni kati ya miezi sita hadi miaka 15 kwa kutegemea aina ya mradi
wa kilimo pamoja na makadirio ya hesabu
Mboje aliongeza kuwa mikopo hiyo huwa na kipindi cha rehema kinachotolewa
kulingana na kipindi cha kukomaa kwa mazao husika pamoja na makadirio ya
mtiririko wa fedha ambapo kipindi cha juu cha rehema ni miaka 3 kwa mazao ya
muda mrefu na mwaka mmoja kwa mazao ya muda mfupi.
“Benki ya Maendeleo TIB ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa
malengo ya kuwezesha upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu na wa kati kwa ajili
ya maendeleo ya kiuchumi hapa nchini,” alieleza Mboje.
Benki ya Maendeleo TIB ilishiriki maonesho hayo ya Wiki ya Huduma
za Fedha yenye kauli mbiu ‘Elimu ya fedha kwa maendeleo ya watu’ ili kutoa ya
kuujulisha umma kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na benki hiyo.
Comments
Post a Comment