Wadau kuujadili uhuru wa habari Zanzibar

NA MWANDISHI WETU KAMATI ya maandalizi ya siku ya uhuru wa habari duniani Zanzibar, imeeleza kuwa maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani yanategemewa kufanyika Mei 23, mwaka huu. Taarifa iliyotolewa kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo inayoundwa na Baraza la habari Tanzania (MCT ) Ofisi ya Zanzibar , Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania Zanzibar (TAMWA - ZNZ), Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo (WAHAMAZA) na Klabu ya Waandishi wa Wabari Zanzibar (ZPC), Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Mzuri Issa, alisema maadhimisho hayo yatafanyika ukumbi wa ZSSF Kariakoo Zanzibar. Alisema maadhimisho hayo yatahudhuriwa pamoja na waandishi wa habari, wadau mbali mbali wa habari na wawakilishi kutoka asasi za kiraia za ndani ya Zanzibar. Dk. Mzuri alisema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yamebeba ujumbe wa ‘Uhuru wa vyombo vya habari na mageuzi ya sera na sheria za habari Zanzibar’ ambao ni muhimu katika kukuza na kuimarisha kada ya ha...