TAMWA yawataka waandishi kuhimiza mabadiliko kijinsia michezoni.
NA AMINA MCHEZO
WAANDISHI wa habari wmeatakiwa kutumia kalamu zao kuwavuta na kuonesha fursa zilizopo Kwa wanawake michezoni.
Akifungua mafunzo ya habari za jinsia na michezo kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar, Dk. Mzuri Issa Ali katika ofisi za chama hicho Tunguu, mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema ushirikishwaji wa wanawake katika michezo ni mdogo kutokana na kutozungunzwa fursa katika vyombo vya habari.
Amebainisha kuwa TAMWA kushirikiana na wadau mbalimbali wamesaidia kwa kiasi kikubwa kuondosha mifumo kandamizi kwa wanawake hasa katika nafasi za uongozi hivyo kwa sasa wameona kuna haja kuelekezwa nguvu michezoni.
Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo ambae pia ni Mjumbe wa bodi ya TAMWA Zanzibar, Hawra shamte amesema wanawake wana haki ya kushiriki katika michezo bila ya kuvunja mila na tamaduni zao.
Hawra amewatoa hofu wanawake wanaohitaji kushiriki katika michezo na kusema wapo wanawake waliofanikiwa kimataifa Zaid kimichezo na bila kuvunja tamaduni Kwa kuvaa mavazi ya staha.
Wakitoa maelekezo katika mafunzo hayo mwakilishi kutoka CYD, Rahma Juma na Mwakilishi wa shirika la GIZ, Hijja Mohamed Ramadhan, wamesema mafunzo hayo yataibua changamoto wanazokumbana nazo wanamichezo wa kike wakati wakiwa michezoni na kupatiwa ufumbuzi.
Mafunzo hayo ya siku tano ya kuwajengea uwezo waandishi wa habar yalioandaliwa na tamwa Zanzibar Kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), CYD yametokana na mradi wa maendeleo ya michezo unaofadhiliwa na taasisi ya serikali ya Ujerumani GIZ.
Comments
Post a Comment