Vyama tisa vyapongeza CCM, ACT kuunda SUK

NA MWANDISHI WETU

VYAMA vya upinzani Zanzibar vimempongeza Rais wa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa hotuba aliyoitoa wakati wa hafla ya kumuapisha Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamo wa kwanza wa Rais wakisema imeakisi dhamira yake ya kujenga Zanzibar mpya.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini ambae pia ni katibu wa umoja huo unaoundwa na vuyama tisa vya siasa, Ameir Hassan Ameir, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habar na kueleza kuwa kama kufanya hivyo pia ni kuitii katiba na sheria ya Zanziar.

Alisema kitendo cha kumteua na kumuapisha kiongozi huyo wa chama cha ACT Wazalendo pia kunatimiza ahadi ya dk. Mwinyi aliyoitoa wakati wa kampeni na baada ya kuapishwa kuwa atashirikiana na vyama vya siasa ili kuunda serikali ya kitaifa itakayoleta maendeleo ya haraka kwa wananchi wake.

“Kwa heshima zote Rais (Dk. Mwinyi) alimteuwa na kumuapisha Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamuwa wa Kwanza wa Rais, hivyo kwa hatua hiyo sisi kama vyama vya siasa tunampongeza sana kwa kutimiza matakwa ya katiba,” alisema

Aidha alisema umoja huo utatekeleza kwa vitendo yale yote aliyoyazungumza Rais ikiwemo wajibu wao kama vyama vya siasa katika kuleta maendeleo ya nchi.

Ameir aliwataka viongozi wote wajue wajibu wao na kwa pamoja wamuunge mkono Dk. mwinyi katika kuijenga nchi na sio kuibomoa, kwani uwajibikaji wa Rais unaonesha azma njema ya kuiletea maendeleo ya haraka nchi.


KATIBU wa Umoja usio rasmi wa vyama vya upinzani Zanzibar , Ameir Hassan Ameir, akizungumza na waandishi wa habarimjini zanzibar. 

Nae Katibu wa Chama cha UDPD, Hamad Mohammed Ibrahim, alimpongeza Dk. Mwinyi kwa uzalendo aliouonesha wa kumteua kiongozi huyo na kwamba kufanya hivyo kutawaunganisha wananchi wa Zanzibari.

“Zanzibar watu wake wapo kitu kimoja, hivyo uamuzi wad k. mwinyi kuridhia kuunda serikali ya pamoja bila kujali tofauti za kisiasa ni jambo jema na kila mwananchi anatakiwa kumuunga mkono ili kuleta maendeleo ya nchi,” aliongeza Hamad.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama cha DP, Peter Agaton, alisema ameridhishwa na utendaji kazi wa Dk. Mwinyi na kuahidi wataendelea kushirikiana nae katika utekelezaji wa mipango yake ya kuiletea maendeleo zanzibar.

“Hata kama hatuna nyazifa yeyote katika serikali, bado kama viongozi wa kisiasa tuna wajibu wa kuhakikisha mipango ya kiongozi aliechaguliwa inatekelezeka,” aliemeza Agaton.

Aidha aliwataka viongozi na watendaji wa taasisi mbali mbali za umma kuendelea kutekekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na muundo wa utendaji wa Dk. Mwinyi ambae aliapa kupambana na uzembe, rushwa na uhujumu uchumi.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango