WADAU  WATAKA KONGAMANO  KUONDOA HOFU KUTOWEKA KWA AMANI
Katika kutekeleza mradi wa kuimarisha amani, uvumivu wa kisiasa na utamaduni wa kupokea tofauti za maoni (peace, tolerance and differences on opinion) unaofadhiliwa na shirika la Internews, Jumatatu Novemba 30, 2020 Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) iliandaa mkutano wa wadau wa amani na uchaguzi uliojadili juu ya namna ya kuendeleza amani baada ya uchaguzi na kufikia maazimio kwamba wadau wote wanapaswa kushirikiana kutafuta suluhu itakayoondoa hofu ya kupotea kwa amani hasa katika kipindi cha uchaguzi.


Mwenyekiti wa ZPC Abdalla Mfaume (alieipa mgongo kamera) akiongoza mkutano wa wadau wa amani uliofanyioka katika ukumbi wa kitengo cha uzazi shirikishi Kidongo Chekundu Novemba 30, 2020.


Mchungaji wa kanisa Anglican Zanzibar, Father Philip Munguti akichangia mada katika mkutano wa wadau wa amani uliojadili namna ya kuimarisha amani, uvumilivu wa kisiasa na utamaduni wa kupokea maoni tofauti.


Mjumbe wa Chama cha Wanahabari Wanawake, Maryam Chum, akichangia mada katika mkutano wa wadau wa amani uliojadili namna ya kuimarisha amani, uvumilivu wa kisiasa na utamaduni wa kupokea maoni tofauti ambapo alisisitiza umuhimu wa kutunza amani kama njia ya kuepusha vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.


Afisa Mrajis kutoka Ofisi ya Mrajis wa Asasi za Kiraia, Mwanabaraka Saleh, akizungumza katika mkutano wa wadau wa amani uliojadili namna ya kuimarisha amani, uvumilivu wa kisiasa na utamaduni wa kupokea maoni tofauti ambapo alipongeza juhudi zilizochukuliwa na asasi za kiraia kutoa elimu ya uraia na mpiga kura katika uchaguzi wa Oktoba 28, 2020.


Mkuu wa Usalama Barabarani (RTO) wa mkoa wa Mjini Magharibi, Issa Milanzi, akizungumza katika mkutano wa wadau wa amani uliojadili namna ya kuimarisha amani, uvumilivu wa kisiasa na utamaduni wa kupokea maoni tofauti ambapo mbali ya kupongeza kazi iliyofanywa na wadau katika kuhimiza amani na kushauri kuendelezwa kwa ushirikiano baina ya wadau na wananchi kunda amani ya Zanzibar.

Afisa Mipango wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Abdul-latif Mohammed, akizungumza katika mkutano wa wadau wa amani uliojadili namna ya kuimarisha amani, uvumilivu wa kisiasa na utamaduni wa kupokea maoni tofauti, alieleza namna ofisi yake ilivyochukua hatua za kuelekeza masheikh, maimamu na waumini wa dini ya kiislamu kuhubiri na kulinda amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi kama sehemu ya ibada.

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), Tabia Mohammed, akiakhirisha mkutano wa siku moja wa  wadau wa amani na uchaguzi uliojadili namna ya kuimarisha amani, uvumilivu wa kisiasa na utamaduni wa kupokea maoni tofauti uliofanyika katika kitengo cha uzazi shirikishi Kidongo Chekundu. kushoto ni Naibu Katibu Mkuu ZPC Mwajuma Juma na kulia ni Katibu Mkuu Mwinyimvua Nzukwi.



 

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango