Dk. Mwinyi awaagiza Makatibu Wakuu kusimamia mapato, matumizi

NA MWAMDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Makatibu wa Wakuu wa wizara za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kusimamia uwajibikaji, ongezeko la mapato na kuondoa urasimu kwenye wizara zao.

Dk. Mwinyi ametoa maagizo hayo kwenye hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni wakiwemo makatibu wakuu, manaibu makatibu wakuu, Mwenyekiti, Wajumbe kamisheni ya utumishi na mkuu wa wilaya ya Magharib ‘A’

Alisema Makatibu Wakuu ndio wasimamizi wakuu wa utendaji kwenye wizara, hivyo wakasimamie uwajibikaji, utoaji huduma bora kwa wananchi, wakasimamie mapato na kuondosha urasimu.

Alisema inashanga hadi leo zipo baadhi ya wizara maduhuli ya serikali yanakusanywa kwa fedha tasilimu, wakati ikizingatiwa tekolojia hiyo imepitwa na wakati na kwamba fedha za serikali zinatakiwa zikusanywe kwa njia ya mtandao. 

"Nataka mkahakikishe fedha na maduhuli ya serikali yanakusanywa kama ilivyotakiwa kwani kumekuwepo fedha zinakusanywa kwa mikono, nataka fedha zikusanywe kwa njia benki kwani maeneo mengi yanayokusanya fedha kwa njia za mtandao tumeziona zinaingia serikalini”, alisema.

Katika hatua nyengine Dk. Mwinyi aliwaagiza makatibu hao kuhakikisha wanaondoa aina zote za ubadhilifu katika wizara zao na kutumia fedha kwa mujibu wa muongozp wa bajeti iliyopo.

“Makatibu wakuu mtambue nyie ndio maamlaka ya nidhamu na uwajibikaji wa wafanyakazi wa wizara, hata waziri akitaka kufanyakazi dhidi ya mfanyakazi atakuagiza katibu mkuu uchukue hatua, hivyo mhakikishe wafanyakazi wanaotukwamisha wasiendelee kufanya hivyo na kuwapa haki zao kwa wakati waliochini yenu”, alisema.

Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimwapisha Abeda Rashid Abdullah kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto.

Alisema nchi haiwezi kwenda kama wengine wanajenga na wengine wanabomoa akimaanisha wanaofisi mali za umma, hivyo serikali itaendelea kuwabana wate wanaojihuisha na vitendo vya ufisadi kwani wanachelewesha maendeleo.

Alisema kuna ubadhirifu mkubwa uliofanywa na kwamba waliohusika lazima wasimamishwe kazi na kupicha uchunguzi na ikibainika kuwa hawana hatia serikali haitawadhulumu lakini ikibainika wana hatia hatua zitachukuliwa dhidi yao.

Pamoja na hayo, aliwasisitiza kusimamia safari za kikazi kwa wafanyakazi na kuacha upendeleo pamoja na fursa za masomo kwani unasababisha kuondosha ari kwa kufanyakazi.

Akizungumzia eneo la manunuzi, Dk. Mwinyi, aliwataka wasimamie kamati za manunuzi kwa kuhakikisha kinachonunuliwa kina thamani ya fedha zinazotolewa, kwani kuna tatizo kwamba vitu vingi vinavyonuliwa havina thamani ya fedha za manunuzi zilizotumika.

Aidha alisema kuwa miradi mbalimbali inafeli kutoka na matumizi mabaya ya fedha za serikali, ambapo hatua zinazochukuliwa kwa sasa hatoonewa mtu na hatua zinachukuliwa kwa kuona hali inakaa vizuri. 

Hata hivyo alisema amepunguza idadi ya manaibu makatibu wakuu ili kupunguza ukubwa wa serikali na kupunguza matumizi makubwa ili fedha zinazopatikana zielekezwe kwenye maendeleo ya wananchi.

Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimwapisha Suzan Peter Kunambi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi 'A'.

Katika hafla hiyo Dk. Mwinyi aliwaapisha Makatibu Wakuu wa wizara zote pamoja na baadhi ya Manaibu Makatibu wakuu katika baadhi ya wizara, Mwenyekiti na wajumbe wa Kamisheni ya Utumishi Serikalini pamoja na Suzan Peter Kunambi alieapa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharib ‘A’, Unguja.

 

 

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango