Maalim Seif: Viongozi tendeni haki kwa wote
NA MWANDISHI WETU
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif
Hamad, amewata viongozi kutenda haki kwa Wazanzibar wote bila ya kujali tofouti
zao.
Alisema kama wananchi na
viongozi wao watashirikiana itakuwa chachu ya kusukuma mbele gurudumu la maedeleo
miongoni mwa Wazanzibari.
Maalim Seif alisema hayo katika
msikiti wa Jumuiya ya Waarabu, Rahaleo Unguja, alipoungana na waumini wa dini ya
Kiislam kkatika swala ya Ijumaa.
Aliwataka viongozi waliochaguliwa na walioteuliwa kupiga vita
ubaguzi wa aina yoyote katika kuwahudumia wananchi.
“Tukifanyakazi kwa pamoja nakuhakikishieni maendeleo ni rahisi
sana,” alisema Malim Seif.
Sambamba na hilo amewataka waumini dini ya Kiislam kuiombea dua Zanzibar
ili umoja uliopo udumu.
Akizugmzia kuhusu ajira uwepo wa utulivu ni muhimu kwa
ushiriiana an sekta binafsi kuondoa changamoto ajira Viwani Zanzibar.
“Kama tukuvutana tutachelewa
kupata maedeleo lakini sisi Wazanzibar tumelijua hilo ndio maana tukawa na Serikali
ya Umoja wa Kitaifa,” alieleza Maalim Seif.
Alieleza kuwa changamoto ya
ajira ni kubwa ambayo huipata wahitimu wa vyuo vya elimu ya Juu mbali mbali
Tanzania.
Alisema Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar imejipanga kutatua changamoto ya ajira inayowakabili kina mama na vijana
na kuwataka wananchi wote kushiriki kwa hali na mali katika shuhuli za Maendeleo
hapa nchini.
Comments
Post a Comment