Dk. Mwinyi  abainisha ufanisi wa serikali ndani ya siku 100 akiwa ofisini

NA MWANDISHI MAALUM

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi, amesema katika kipindi cha siku 100 za uongozi wake amefanikiwa kuteekeleza mambo 10 kwa ufanisi zaidi.

Dk. Mwinyi alieleza hayo ikulu mjini Zanzibar wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kutimiza siku 100 tangu aliapishwa Novemba 2 mwaka jana.

Alisema katika kipindi hicho kifupi amefanikiwa kuleta umoja wa kitaifa kwa kuweka maridhiano ambayo yameongeza ushirikiano miongoni mwa wananchi na kule amani na utulivu.

Alisema ameunda serikali yenye muundo wa umoja wa kitaifa ili kondosha yanayotokea kila baada ya uchaguzi mkuu na kwamba mshikamano amani na utulivu utaongeza kasi ya maendeleo ya nchi.

Alifahamisha kuwa apanga kuona vyombo vya sheria vinafanyakazi yake vizuri ikiwemo kuipa nguvu Mamlaka ya Kupambana na Rushwa na Uhujumu (ZAECA), kwani imebaini kuwepo kwa wizi mkubwa katika Mikoa na Halmashauri.

Alisema katika kulisimamia suala la uwajibikaji alisema atahakikisha uundaji wa bodi, unafanyika kwa kuzingatia taaluma kwani baadhi ya wanaochaguliwa walikuwa hawana sifa kama ilivyojitokeza PBZ.

Alisema katika utawala wake atahakikisha naziba matundu yote ya wizi wa fedha za serikali, kwani hivi sasa kuna watu wameanza kurudisha fedha walizoiba kwneye taasisi za umma.

Kuhusu uwekezaji alisema tayari imeingia mikataba mikubwa ya ujenzi wa bandari ya Mwangapwani itayojengwa kwa mashirikiano na Oman, itayokuwa na uwezo mkubwa wa kubeba makontena, bandari ya mafuta na gesi na chelezo.

Alisema bandari nyengine serikali inakusudia kujenga kwa Mpigaduri itayokuwa inashughulikia wavuvi ukiwemo mradi wa kuimarisha viwanda utaotumia dola 6.3 bilioni utaowashirikisha wawekezaji kutoka nchi mbali mbali, kwa vile serikali imeona isichukue mkopo.

Upande wa bandari ya Malindi, Dk. Mwinyi alisema, serikali inakusudia kuifanya kuwa ya kitalii kwa vile ipo katika eneo la Mjimkongwe ambao ni mji wa utalii.

Eneo jengine ambalo Dk. Mwinyi alilitaja ni suala la kuimarisha mradi wa nishati kwa kuongeza megawati 350 na tayari wameanza mazungumzo na benki ya Dunia  kuwekeza umeme wa jua KV 32.

Alisema serikali imefanikiwa kukusanya mapato ya miezi sita katika kupindi cha mwezi mmoja kwenye bandari ya Malindi, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 4.5 zilikusanywa mwezi Disemba mwaka jana.

Alisema upande wa uwanja wa ndege serikali inategemea kufanya vizuri baada ya jengo la Terminali III kunalizika kwani wanakusudia kuanzisha kiwanja cha Mizigo.

Dk. Mwinyi alisema sekta ya biashara nayo imepiga hatua kwa kuweka mazingira bora kwa kupanga kuondoa badhi ya kodi pamoja na kuanza kazi kwa wanyabiasha waliohamishwa Kibanda Maiti.

Upande wa sekta ya Afya, Dk. Mwinyi, alisema wataziangalia sera, Sheria na kanuni ili kuifanya ifanye vizuri, pamoja kuangalia kuanzisha utaratibu wa bima ya afya.

Kuhusu Mamlaka ya Maji (ZAWA), Dk. Mwinyi alisema tayari wananchi wameanza kupata huduma ya maji katika maeneo ambayo waliikosa pamoja na huduma ya umeme baada ya serikali kupunguza gharama, kwani watu 320 wameshafungiwa mita hizo pamoja na ujenzi wa barabara kwa kuziba mashimo na utatuzi wa migogoro  ya ardhi.

Akizungumzia utawala Bora, Dk. Mwinyi alisema tayari kuna wafanyakazi 80 wamesimamishwa kazi kutokana na wizi uliojitokeza.

Akizungumzia udhalilishajia alisema tayari ameziagiza taasisi zinazohusika na kusimamia kesi kwa kuanzisha Mahakama pamoja na kuwaondolea dhamana watuhumiwa wa kesi hizo.

Kuhusu sekta binafsi, Dk. Mwinyi alisema, inaenda vizuri kutokana na kuwapo muitikio ni mkubwa zikiwemo Mabenki ya CRDB na NMB.

Hata hivyo Dk. Mwinyi amekubali kufanya mazungumzo na Jukwaa la Wahariri, na kuagiza Mawaziri kufanya mazungumzo na Waandishi kila mwezi, ili kujua mafanikio na changamoto za serikali.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango