Kijichi wapongeza kasi ya awamu ya nane

NA MWANDISHI WETU

WANACHAMA na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), jimbo la Bububu wametakiwa kuendeleza ushirikiano walionao ili kuongeza kasi ya maendeleo ya jimbo hilo na watu wake.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Kamati ya siasa ya wilaya ya Magharibi 'A' ambae pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Suzan Peter Kunambi, alipokuwa akizungumza na wanachama hao katika tawi la CCM Kijichi.

Alieleza kuwa serekali ya awamu ya nane imelenga kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hivyo ushirikiano baina ya viongozi, wanachama na wananchi ni muhimu ili kufikia malengo yaliyowekwa.

“Mnaposhikamana na kushirikiana kama ilivyo katika jimbo lenu, mnaweza kwenda mbali zaidi na kufikia maendeleo makubwa katika kipindi kifupi. Na hilo ndilo lengo la serikali inayoongozwa na Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,” alieleza Suzan.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya ambae alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kaskazin Unguja, Ayuob Muhammed Mahmoud katika mkutano huo, aliwataka wanachama wa chama hicho kuendelea kujitolea na kukichangia chama chao ili kiweze kujitegemea na kufanikisha mipango ya maaendeleo iliyojiwekea.

“Niwapongeze wanachama wa tawi hili kwa kufikiria kuwa na ofisi ya kisasa yenye miradi ya kujiongezea kipato. Huo ndio ubunifu unaohimizwa na mimi sitawaacha hivi hivi, nitashirikiana nanyi kuhakikisha lengo linafikiwa,” alisema suzan na kuwahimiza kupiga vita ubadhirifu, ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

Akisoma risala kwa niaba ya wanachama wenzake, katibu wa ccm tawi la kijichi, Lemi Shija, alieleza kuwa wapo tayari kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, katika mapambana na vitendo dhidi ya uzalilishaji kwa wanawake na watoto.

Aidha waliipongeza serikali ya awamu ya nane kwa kutimiza siku 100 kwa mafanikio lakini pia ccm iliyotimiza miaka 44 ikiwa madarakani, umoja na mshikamano pande zote mbili za muungano wa Tanzania.

“Kwa ujumla sisi wanachama wa CCM tawi la Kijichi, tunampongeza Rais Dk. Mwinyi (Hussein Ali Hassan) kwa jinsi alivyoanza kazi ya kuijenga Zanzibar mpya na tuaanihidi kumuunga mkono kwa kuhakikisha tunakemea rushwa, uhujumu uchumi na vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto,” alieleza Lemi.

Nae diwani wa wadi ya Dole, Juma Wiliam Sungwa, alieleza kuwa mkutano huo uliitishwa kuwapongeza wanachama wa chama hicho na wananchi kwa kukipa ushindi wa kishindo chama hicho lakini pia kuchangia ujenzi wa  ofisi za chama hicho.

Mkutano nhupo ambao ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo mwakilishi wa jimbo hilo, ambae pia ni waziri wan chi ofisi ya rais, kazi, uchumi na uwekezaji, mudrik ramadhan soraga, uliambatana na harambee ya kuchangia ujenzi wa tawi hilo ambapo jumla ya shilingi 5,410,000 taslimu na ahadi zilikusanywa.

MAELEZO YA PICHA:

Mkuu wa wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan Peter Kunambi (wa pili kushoto), akiongozana na Mwakilishi wa jimbo la Bububu, Mudrik Ramadhan Soraga (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM jimbo hilo, Yumeni Kibwana Nzukwi, alipowasili katika viwanja vya skuli ya sekondari Wazazi Dole, kabla ya kuhutubia wananchi na wanachama wa CCM wa tawi la Kijichi. (PICHA NA MPIGA PICHA WETU).

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango