Taifa limepoteza kiongozi jasiri, mzalendo – Dk. Mwinyi
NA MWANDISHI WETU
MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amefariki
dunia.
Akitangaza kifo cha mwanasiasa huyo aliezaliwa Oktoba 22, 1943, Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, alieleza
kuwa Maalim Seif amefariki dunia jana katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa
akipatiwa matibabu.
“Majira ya saa 5:26 asubuhi, makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Maalim
Seif Sharif Hamad. Maalim amefariki wakati akiendelea na matibabu katika
hospitali ya muhimbili alipokuwa amelazwa tokea tarehe 9 mwezi huu,” alieleza
Dk. Mwinyi katika taarifa yake kupitia televisheni ya Shirika la Utangazaji
Zanzibar (ZBC).
Aidha Dk. Mwinyi alitoa pole kwa familia ya marehemu, viongozi na
wanachama wa chama cha ACT Wazalendo, wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa
ujumla akiwataka kuendelea kuwa watulivu na wavumilivu.
Maalim seif ambae hadi mauuti yanamkuta alikuwa mwenyekiti wa chama cha
act wazalendo, alikuwa ni miongoni mwa wanachama na viongozi waanzilishi wa
chama cha wananchi CUF mwaka 1992.
Aidha kiongozi huyo, aliekihama chama hicho machi 18, 2019 na kujiunga na
ACT Wazalendo, aliasisi maridhiano ya kisasa ya Zanzibar yaliyoapelekea
mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya 1984 yaliyoanzisha serikali ya umoja
wa kitaifa Zanzibar.
Baada ya kutolewa kwa tangazo hilo, viongozi na wananchi mbali mbali
walijitokeza na kutoa salamu za pole kwa familia, Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Watanzania na Wazanzibari.
Miongoini mwa viongozi hao ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.
John Pombe Magufuli, aliemtaja marehemu kuwa ni miongoni mwa viongozi wazalendo
na kumuombea dua kwa mwenyezi mungu.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad. Natoa pole kwa Dk. Mwinyi,
familia, Wazanzibari na Watanzania wote. Mungu amweke mahali pema, aamini,”
alieleza Dk. Maguli katika ukurasa wake wa ‘twitter’.
Comments
Post a Comment