Wajumbe wa ACT Wazalendo wala kiapo

NA MWANDISHI WETU

WAJUMBE wapya watano wa Baraza la Wawakilishi Zaznzibar, wameapishwa katika siku ya kwanza ya mkutano wa pili wa baraza hilo ulioanza Februari 10, mwaka huu.

Spika wa baraza hilo Zubeir Ali Maulid, amewaapisha wajumbe hao kutoka kutoka chama cha ACT  Wazalendo akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui.

Walioapishwa ni Mwanasheria wa Omar Said Shaabani, Nasor Ahmed Mazrui ambao ni wajumbe wa baraza hilo waliotokana na uteuzi wa Rais wa Zanzibar.

Wajumbe wengine walioapishwa ni Habib Ali Mohamed, Mwakilishi wa Mtambwe, Hassan Hamad Omar kutoka jimbo la Kojani na Kombo Mwinyi Shehe, kutoka jimbo la Wingwi.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe, Habib Ali Mohamed, alisema atafanya kazi hiyo kwa kuwakilisha wananchi bila ya ubaguzi pamoja na kutoa hoja zenye maslahi kwa maisha yao.

Alisema wawakilishi wote wana lengo linalofanana na ni vyema wakashirikiana kwa pamoja ili lengo la serikali litimie katika kuwatumikia wananchi.

Wakati huo huo, Baraza hilo limefanya uchaguzi kwa wajumbe watano wa baraza hilo watakaokwenda kuliwakilisha baraza katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waliochaguliwa ni Ameir Abdalla, Bakari Hamadi, Khamis Kombo, Mwatatu Mbarak Khamis, Suleiman Haroub.

Kwa upande wa uchaguzi wa Umoja wa Wanawake wa Baraza la Wawakilishi, (UWAWAZA) wajumbe hao walimchagua Saada Salim Mkuya, kuwa Mwenyekiti, Mwantatu Mbarak Khamis kuwa Makamu Mwenyekiti na Anna Atanas Paul kuwa katibu wa umoja huo.

Vile vile, Wawakilishi hao waliwachagua Wajumbe wa kamati Tendaji ya Jumuiya hiyo akiwemo Bahati Khamis Kombo, Mwajuma Kassim Makame, Rukia Ramadhan na Salha Mohamed Mwinjuma.

 

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango