MAKABIDHIANO YA MSAADA WA MAGARI YA USAFI YALIYOTOLEWA NA SHIRIKA LA MISAADA KIMATAIFA LA ROMANIA (RoAID) KWA MANISPAA NA MABARAZA LA MJI YA ZANZIBAR
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Masoud Ali Mohammed, akiwasili katika viwanja vya ofisi ya kampuni ya Rom Solutions, Kisauni, katika hafla ya makabidhiano ya magari ya usafi kwa ajili ya manispaa za Mjini Magharibi na Baraza la Mji wa Chakechake zilizotolewa na shirika la misaada ya Romania (RoAID). (PICHA NA MZEE GEORGE).
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Masoud Ali Mohammed, akihutubia katika hafla ya makabidhiano ya magari ya usafi kwa ajili ya manispaa za mkoa wa Mjini Magharibi na Baraza la Mji wa Chakechake zilizotolewa msaada na Shirika la misaada ya Kimataifa la Romania (RoAID). (PICHA NA MZEE GEORGE).
BAADHI ya viongozi na watendaji wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, wakifuatilia hotuba ya Waziri wa wizara hiyo Masoud Ali Mohammed wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari ya usafi, msaada uliotolewa na Shirika la Misaada la Romania (Ro AID), iliyofanyika jana katika ofisi za Rom Solution, Kisauni. (PICHA NA MZEE GEORGE).
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Masoud Ali Mohammed (kulia), akisaini nyaraka za magari ya kubebea taka katika hafla ya makabidhiano ya magari ya usafi kwa ajili ya manispaa za Mjini Magharibi na Baraza la Mji wa Chakechake zilizotolewa na shirika la misaada ya Romania (RoAID). (PICHA NA MZEE GEORGE).WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Masoud Ali Mohammed, akimkabidhi mmoja ya madereva wa magari ya usafi funguo na cheti maalum baada ya kushiriki mafunzo ya uendeshaji magari hayo yaliyotolewa na Shirika la Misaada la Romania (RoAID), kwa manispaa za mkoa wa Mjini Magharibi na Baraza la Mji Chakechake. (PICHA NA MZEE GEORGE).
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Masoud Ali Mohammed (katikati), akibadilishana mawazo na Afisa Sheria wa Shirika la Misaada Kimataifa la Romania (RoAID), Florian Valentin Petrache, baada makabidhiano ya magari manne ya usafi yaliyotolewa na shirika hilo hafla iliyofanyika katika ofisi za kampuni ya Rom Solution, Kisauni. (PICHA NA MZEE GEORGE).
Comments
Post a Comment