ZPC, CPS Ltd zaazimia kuimarisha ushirikiano
NA
MWANDISHI MAALUM
KATIKA kuimarisha mahusiano na ushirikiano kati ya Klabu ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) na wadau wake, viongozi wa klabu wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Tabia Makame Mohammed (Februari 7, 2022) wametembelea na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CPS Ltd Tobias Dietzold.
kampuni ya CPS Ltd inayojenga Mji wa Maendeleo
wa Fumba (Fumba Town Development) uliopo Nyamanzi, wilaya ya Magharibi ‘B’,
Unguja imekuwa na mahusiano ya karibu ya kikazi na klabu hiyo toka mwaka 2016 ambapo zimekuwa zikishirikiana katika mambo mbali mbali.
Katika mazungunzo yao, pande mbili hizo
zimebadilishana mawazo na kukubaliana kuimarisha mahusiano na kushirikiana
katika utekelezaji wa malengo na majukumu ya taasisi hizo hususani kutoa elimu
kwa jamii juu ya umuhimu wa kuwa na makaazi bora kama ilivyo katika sera na
mipango yanserikali.
Aidha
Tobias aliipongeza ZPC kwa kuendelea kuwa karibu na kampuni yao na kuahidi
kushirikiana na vyombo vya habari vya Zanzibar kuijumisha jamii dhamira ya
uwekezaji wanaoufana nchini.
"Tunashukuru
siku zote mmekuwa pamoja nasi na kutusaidia kutambulisha mradi wetu ambao upo
kwa ajili ya Wazanzibari ili kukabiliana na changamoto ya ufinyu wa ardhi na
mahitaji ya makaazi," alieleza Tobias.
Alieleza
kutokana na ongezeko la watu, kumekuwa na majitaji makubwa ya makaazi hivyo ipo
haja ya nchi kuwa na mikakati ya kuhifadhi aradhi kwa kujenga nyumba imara
katika eneo dogo.
Nao
viongozi wa klabu hiyo walieleza kufurahishwa kwao na maendeleo ya
utekelezaji wa mradi huo unaohusisha
nyumba za chini na ghorofa.
Aidha
viongozi hao walipata taarifa mbali mbali zinazohusu utekelezaji wa mradi huo
na kuwaomba kutumia vyombo vya habari kutangaza mradi huo.
PICHA
Makamu Mwenyekiti wa ZPC, Tabia Makame Mohammed (kulia) akiongoza kikao kati ya viongozi wa klabu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya CPS Limited, Tobias Dietzold, kilichofanyika katika ofisi za kampuni hiyo Nyamanzi.
Wajumbe
wa Kamati Tendaji ya ZPC wakiongozwa na Afisa Masoko na Biashara, Paul Wangoma (kulia) walipotembelea maeneo yanayoendelea na ujenzi katika Mji
wa Maendeleo wa Fumba (FTD) walipofanya ziara na mazungumzo na uongozi wa
kampuni ya CPS Ltd.
Comments
Post a Comment