Msisambaze habari zilizothibitishwa - Mfaume

NA MWANDISHI MAALUM

WATUMIAJI wa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari nchini wametakiwa kutosambaza habari zisizothibitishwa ili kuepuka kuingia katika migogoro ya kisheria.

Mjumbe wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abdallah Abdulrahman Mfaume, (pichani aliesimama) alitoa wito huo wakati akifungua mkutano wa majadiliano iliyowakutanisha wadau mbali mbali wa habadi na jumuiya za kiraia zinazohusika na maendeleo ya vijana Zanzibar.

Alisema maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani yameongeza wigo wa utoaji na usambaji wa habari na taarifa hivyo ipo haja ya kuchukuliwa kwa hatua za tahadhari ili kuepusha madhara kwa jamii.

Alisema kazi ya usambazaji na utoaji wa habari nchini unasimamiwa na sheria, kanuni na muongozo hivyo kuna umuhimu wa kuzingatiwa wwledi katika dhana ya uandishi wa habari.

"Upashanaji wa habari katika nchi yeyote unasimamiwa na sheria na kanuni na sio kila mtu anaweza kuifanya. Hivyo ni vyema tukawa na tahadhari tunapotuma habari na tunapotumia mitandao ya kijamii," alieleza Mfaume.

Aidha aliipongeza taasisi ya jukwaa la vijana Zanzibar (ZYF), kwa kuendelsha mafunzo na kmikutano ya majadiliano kamahiyo ambayo husaidia kupatikana elimu na maoni muhimu.

Aliwaomba washiriki wa majadiliano hayo kutoa maoni yatakayosaidia kuimarisha sera, sheria na miongozo inayotolewa na taasisi zinazosimamia mwenendo wa upashanaji habari ili kutanua wigo wa uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza.

Kwa upande wake mwendeshaji wa majadiliano hayo, mshauri wa vyombo vya habari na mkufunzi katika chuo kikuu cha Zanzibar (ZU), Suleiman Seif Omar, alieleza kuwa pamoja na serikali kuweka uhuru wa habari, imeweka vyombo na sheria ambazo husimamia mwenendo na matumizi ya uhuru huo.

Alisema katika kusimamia sekta ya habari, kuna sheria nyingi ambazo nyengine zina muda mrefu hivyo ipo haja ya kufanyiwa marekebisho ili ziendane na wakati uliopo.

Aidha baadhi ya washiriki wa mkutano huo walieleza haja ya kuwekwa miundombinu rafiki ya upashanaji wa habari ikiwa ni pampja na vyombo vyenye mamlaka kutominya uhuru wa habari na kujieleza.

Walisema ili kufiukia maendeleo ya haraka, kuna umuhimu kwa wadau wa habari kukaa pamoja na kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya utoaji na upatikanaji wa habari ili kuwanufaisha wananchi ambao ni wateja.

Wakizungumzia matumizi ya mitandao ya kijamii kama vyombo vya kupokea na kusambaza habari, walisema ipo haja kwa mamlaka zinazhusika kuangalia namna ya kudhibiti watu wanaotumia vibaya mitandao hiyo badala ya kuzuia matumizi kwa watumiaji wote.

“Kwa mfano wakati wa uchaguzi, TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania) walizuia mitandao jambo ambalo lilituathiri wengi ambao huitumia mitandao ya kijamii kwa shuguli za biashara au kazi,” alieleza shadida omar kutoka jumuiya ya ZAFAYCO.

Akitole ufafanuzi baadhi ya hoja, Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Omar Said Ameir, alieleza kuwa hatua zinazochukuliwa kudhibiti watu wanaotumia vibaya mitandao, zinalenga kulinda amani, mila na silka za nchi.

“Tunapochukua hatua, hatudhamiri kumuumiza mtu bali kulinda amani ya nchi na hufanya hivyo kwa kuzingatia sheria baada ya kuwaonya wahusika,” alieleza Omar na kuwataka wasambazaji wa maudhui mitandaoni kusajili mitandao yao kabla ya machi 15, mwaka huu.

Mkutano huo ulishirikisha wadau mbali mbali wakiwemo wawakilishi kutoka vyama vya siasa, vyombo vya habari, asasi za kiraia na watendaji wa serikali, ulijadili matumizi ya sheria katika kuongeza upatikanaji wa uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza na matumizi ya mitandao ya kijamii katika jamii.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango