RoAID yazipatia manispaa gari za kubebea taka
NA MWANDISHI MAALUM
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar
imeeleza kuwa inathamini mchango wa taasisi za kimataifa na washirika wa
maendeleo kwani unachochea kasi ya maendeleo ya nchi na ustawi wa jamii.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wan
chi, ofisi ya rais, tawala za mikoa na idara maalum za SMZ, Masoud Mohammed
Ali, wakati akizungumza katika hafla ya kupokea magari manne ya kubebea
takataka yaliyotolewa na serikali ya Romania kupitia Shirika la Misaada la nchi
hiyo (RoAID).
Alisema msaada huo umekuja wakati
muafaka kwa kuzingatia kuwa serikali ya awamu ya nane imeweka mkazo na
kipaumbele katika usafi wa mji, hivyo msaada huo utaoingeza kasi ya udhibiti na
uondoaji wa taka katika manispaa na halmashauri za miji ya Zanzibar.
Alifafanua kuwa swala la uchafu wa
mji limekuwa kero ya muda mrefu na kupigiwa kelele na viomngozi wakuu wa nchi
hivyo kuna haja ya watendaji wa manispaa kuongeza kasi ya usafishaji wa miji.
“Ikifika mahali hata kiongozi mkuu
wa nchi (Rais) anaonesha kutoridhika na kazi mnazozifanya,viongozi na watendaji
wa manispaa pamoja na halmashauri mnapaswa kujitathmini lakini pia kujiwekea
malengo katika utendaji na usimamizi wa utekelezaji wa majukumu yenu,” alisema
Masoud.
Waziri huyo aliishukuru kampuni ya
Rom Solutions ya Zanzibar na Premium Audit kwa kufanikisha upatikanaji wa
magari hayo jambo ambalo ni mwendelezo wa misaada inayotolewa na taasisi hizo
katika litaongeza ufanisi katika
“Rafiki wa kweli utamjua wakati wa
shida, ninazo taarifa kwamba msaada wenye mnasaba na huu ulitolewa kwa manispaa
na halmashauri zote za Zanzibar, ndio maana ninawapongeza Rom Solutions na
Premium Audit kwa kuratibu upatikanaji wa msaada hii,” alieleza Masoud.
Aidha waziri masoud aliwataka
madereva na viongozi wa manispaa zitakazotumia gari hizo, kuzitunza ili msaada
huo uwe na tija.
Mapema akitoa taarifa fupi ya
msaada huo, mtendaji mkuu wa taasisi ya Premium Audit, Any Ivan – Vasilica,
alieleza kuwa magari hayo ya kisasa yametolewa msaada na shirika hilo kwa watu
wa Zanzibar ili kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na serikali kuimarisha
usafi wa mji.
Alisema licha ya juhudi zinazofanya
na taasisi zinazohusiana na usafoishaji wa miji, bado hali ya udhibiti wa
takataka umekuwa na changamoto jambo ambalo linahitaji mchango wa kila mmoja.
“Toka tumeanza kufanya kazi
Zanzibar mwaka 2018, wakati wote kipaumbele cha kwanza ni mambo yanayoihusu
jamii ya Zanzibar tukiamini kuwa na sisi ni sehemu yake,” alisema Any.
Alisema shirika la RoAid litaendelea
kutoa mchango wake kwa taasisi na serikali ya Zanzibar na kushukuru ushirikiano
inayoupata katika utekelezaji wa majukumu yake.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Zanzibar, Said Salmin Ufuzo, alieleza kuwa gari hizo
zenye uwezo wa kukusanya takataka zitatolewa kwa manispaa tatu za unguja na
moja ya pemba ili kuongeza kasi ya uwekaji mji katika hali ya usafi.
Alizitaja manispaa zitakazonufaika
na msaada huo kuwa ni manispaa ya Mjini, Manispaa ya Magharibi ‘A’ na Magharibi
‘B’ kwa Unguja na Baraza la Mji Chakechake Pemba.
“Tunaamini magari haya yataongeza
ufanisi katika shughuli za uzoaji wa takataka kutoka katika vituo vya
kukusanyia na kuzipeleka jaa kuu Kibele,” alieleza Ufuzo.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Rom Solution Kisauni wilaya ya Magharibi ‘B’, madereva waliopewa mafunzo walikabidhiwa vyeti na funguo za magari hayo yaliyogharimu jumla ya Euro 160,000 zilizotolewa na shirika la RoAid.
Comments
Post a Comment