Ayoub ahimiza upatikanaji wa habari sahihi
NA MWAJUMA JUMA
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja
Ayoub Mohammed Mahmoud, ameeleza kuwa upatikanaji kwa habari sahihi na kwa
wakati ni jambo la lazima hivyo wanahabari wanapaswa kwenda na kasi ya ukuaji
wa teknolojia ya habari na mawasiliano.
Ayuob aliyasema hayo alipokutana
na wajumbe wa Kamati Tendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC),
waliyofika ofisini kwake kujitambulisha huko ofsini kwake Mkokotoni mkoani
humo.
Alisema kutokana na mabadiliko ya
teknolojia, jamii imekuwa ikipata habari nyingi ambazo baadhi yao sio sahihi na
kupelekea athari kwa jamii na ikiwemo migogoro na machafuko ya kijamii.
“Kwa tulipofikia, swala la
kupatikana kwa habari sahihi ni jambo la lazima kwani zinapokosekana habari
sahihi hutolewa sizizo sahihi na zinapoifikia jamii athari yake inakuwa kubwa
na tunaweza kupelekea nchi ikaingia kwenye migogoro ikiwemo ya kivita”,
alisema.
Hivyo alisema uwepo wa Klabu ya
Waandishi wa Habari ni faraja kwa sababu ni chombo ambacho kinakwenda
kuiunganisha tasnia ya habari na hatimae kuwanganisha wale wataalamu wenyewe
wakaweza kufanya kazi kwa uweledi na ufanisi.
Alisema kuwa dhamira ya
kuanzishwa kwa chombo hicho ni kuendeleza tasnia ya waandishi wa habari, ambayo
ni muhimu kubwa katika utoaji wa taarifa kwa jamii.
Sambamba na hayo alisema kuwa
akiwa yeye ni mlezi wa taasisi hiyo ana kila sababu ya kuona kwamba programu
ambazo zilisita zinafanyiwa utaratibu wa kufanyika.
“Nikubaliane na nyinyi kwa sasa
kwamba tuna kila sababu ya kuona zile programu ambazo zinaweza kutekelezeka kwa
sasa zinafanyika,” alisema.
Aidha alisema kuwa programu ya
kufundisha uchumi wa bluu ni programu nzuri na wa mkoa walitoa tangazo ambalo
lilizungumzia dhana ya uchumi huo na namna ya
kuweza kummunga mkono rais wa
Zanzibar lakini pia waweze kuifahamu na kuiishi na kuifaidi.
Hivyo alisema dhana hiyo wao
wameitafasiri katika tamasha moja
linaloitwa tamasha la Vyakula vya Pwani Zanzibar , ‘Zanzibar Sea Food
Festival’, ambapo alisema kupitia tamasha hilo anaamini kuwa wadau wanaoamini
uchumi wa buluu wa moja kwa moja na wasio moja kwa moja watafikiwa na
kuunganishwa.
“Kwa hiyo nanyi mutakapokuja
kujifunza dhana ya uchumi wa buluu na sisi tutapata nafasi ya kuwasilisha hoja
yao juu ya tamasha hilo kwa mkoa wao ili waandishi mukaweza kuibeba na
kuipeleka mbali zaidi”, alisema Ayoub mbele ya Katibu Tawala wa mkoa huo Makame
Machano Haji.
Alieleza kuwa anaamini kupitia
dhana hiyo na kupitia sera hiyo ya taifa sasa wananchi walio wengi wataweza
kupata tija na maslahi yaliyo makubwa zaidi kukuwa kwao kiuchumina ustawi wa
jamii kupitia dhana ya uchumi wa buluu.
Aidha alivipongeza vyombo vya
habari vya Zanzibar kwa jinsi vinavyofanya kazi ya kushajihisha umoja na
ushirikiano wa jamii hasa wakati wa msiba wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania marehemu Dk. John Pombe Magufuli.
Awali Mwenyekiti wa klabu hiyo
Abdalla Abdulrahman Mfaume na Katibu Mkuu Mwinyimvua Nzukwi, walimueleza mkuu
huyo wa mko kwamba klabiu hiyo imejipanda kuwaendeleza wanachama wake katika
aina mbali mbali za uandishi ili kukuza weledi.
“Kwa mfano katika robo ya kwanza
ya mwaka tulipanga nkuwafundisha wanachama wetu namna ya kuzitambu, kuziibua na
kuandika habari za uchumi wa buluu tukiamini kwamba watakapoielewa kwa kina
dhana hii, watawasaidia wananchi kunufaika nao,” alieleza Mfaume.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema
ziara hiyo ni kawaida kwa kiongoizi huyo ambae ni Mlezi wa jumuiya yao,
aliahidi kuendelea kushirikia nan a kiongozi huyo na watendaji wake ili
kuhakikisha mafanikio ya pande zote mbili yanapatikana.
Comments
Post a Comment