Mbunge Welezo akemea udhalilisahaji watu wenye ulemavu
NA MWANDISHI WETU
WAZAZI na walezi wenye watoto wenye
ulemavu, wameombwa kutowaficha kwani kufanya hivyo ni sehemu ya udhalilishaji
na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo
la Welezo, Unguja katika hafla ya kukabidhi viti mwendo (wheel chair) kwa watu
wenye ulemavu wa jimbo hilo iliyofanyika katika tawi la CCM Mwendapole, shehia
ya Welezo wilaya ya Magharibi ‘A’.
Alieleza kuwa kushirikishwa kwa
watu wenye mahitaji maalum katika shuguli za kijamii ni miongoni mwa haki za
binadamu hivyo ipo haja ya elimu iendelee kutolewa.
“Watu wenye ulemavu na wenye
mahitaji maalum ni sehemu ya jamii, hivyo tuwatoeni na kuwapeleka skuli ili
kupata elimu lakini pia tuwashirikishe katika mambo mengine ya kijamii,”
alisema Maulid.
Aidha aliwapongeza wananchi wa
jimbo hilo kwa mashirikiano wanayoyatoa kwa viongozi wa jimbo hilo jambo
linalopelekea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa ufanisi.
“Tuendelee kushikamana na
kushirikiana ili tuweze kukamilisha utekelezaji wa ilani ya CCM na mipango ya
nchi yetu kwa wakati,” alieleza Maulid.
Akizungumza katika makabidhiano
hayo, mzee Usinga Makame Suha, alimshukuru kiongozi huyo na kueleza kuwa kiti
hicho kiamsaidia mtoto wake kujumuika na wenziwe katika masomo na michezo.
“naomba wazazi wenzangu wasione
kuwa na motto mwenye ulemavu kama ni mkosi, tuwape nafasi ya kusoma
tusiwafungie ndani,” alieleza usinba baba wa rauhiya.
Nae mzazi wa mtoto Muayar Mussa
Ali, aliiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili iwalinde watoto
wenye ulemavu dhidi ya aina zote za udhalilishaji.
“Kuwaficha ndani watu wenye ulemavu
kwa kuogopa aibu ni udhalilishaji ambao unapaswa kukemewa ili kuuondoa ndani ya
jamii,” alisema Mussa.
Awali akitoa maelezo juu ya
shughuli hiyo, Katibu wa CCM jimbo la Welezo, Mwanakhamis Khamis Idi, aliwapongeza
viongozi wa jimbo hilo kwa kuanza kutekeleza ahadi zao na kuwaomba waendelee
kufanya hivyo katika makundi na maeneo mengine ya jamii.
“Wakati wa kampeni zipo ahadi
zilitolewa na viongozi kama ahadi zao, ninashukuru kwamba umeanza kutekeleza
ahadi hizo na kukijengea uaminifu chama chetu,” alisema Katibu huyo.
Jumla ya shilingi milioni 8.5
zimetumika kununulia viti hivyo vilivyotolewa kwa watoto na watu wazima wenye
ulemavu wa viungo vya miguu na mwili ili kuwaondolea changamoto ya usafiri
kutoka sehemu moja na nyengine.
Comments
Post a Comment