Wanahabari wahimizwa ‘kuilea’ SUK
NA MWAJUMA JUMA
MKURUGENZI wa Chama Cha
Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) ofisi ya Zanzibar, Dk. Mzuri Issa
amesema kunahitajika nguvu ya pamoja ili kuimarisha maridhiano ya kisiasa
yaliyoasisi Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar.
Akizungumza katika mafunzo ya Waandishi wa habari juu ya umuhimu wa Serikali ya
Umoja wa Kitaifa, alisema waandishi wa habari wanapaswa kuchukua jukumu lao na
kuhakikisha lengo la kuanzishwa kwake linafanikiwa.
Alisema kwenye taifa, ustawi na umoja wa wananchi ni nguvu kubwa katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Hivyo alieleza kuwa waandishi wa
habari wana wajibu wa kuacha ushabiki wa siasa bali wajuwe kwamba wao ndio
wanaopaswa kupaza sauti zao ili jamii izidi kujenga matumaini na serikali hiyo.
Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo, Mkufunzi wa Waandishi kutoka Internews,
Ali Haji Mwadini, alisema pamoja na waandishi kufanya kazi katika mazingira
magumu, bado wanajukumu la kuifahamisha jamii hasa wa vijijini kuhusu Serikali
hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa kufa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya 2010 kulichangiwa sana na waandishi wa habari ambao hawakuweza kutimiza majukumu yao katika kuihamaisiha jamii juu ya uwepo wake.
Hivyo alisema ili wasirejee nyuma ni wajibu wao sasa kutumia kalamu zao kwa kuandika mara kwa mara SUK, ambayo wananchi wanaonekana wana matumaini makubwa na serikali hiyo.
Wakichangia mada hiyo baadhi ya waandishi wa habari walisema kufa kwa serikali hiyo 2010 kulitokana na waandishi kuwa na woga, kuingiza utashi wa kisiasa pamoja na kutokujiamini juu ya kuandika habari ambazo zinahusiana na SUK.
Hata hivyo walisema pamoja na uwepo wa serikali hiyo lakini bado wanawoga kwa kuingiza mambo ya nyuma na wengi wao kudhani kwamba ndani ya Serikali hiyo kuna chama cha siasa.
Mafunzo hayo ya siku moja
yaliandaliwa na Chama cha Wandishi wa Habari wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar
kupitia mradi wa kuwajenga kiwezo wanawake katika uongozi (SWIL) unaofadhiliwa
na UN Women.
Comments
Post a Comment