DC Kunambi awaalika wananchi kukimbiza mwenge
NA SHADYA MOHAMED
MKUU wa wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan
Kunambi amesema miradi mitano yenye thamani ya shilingi milioni 619,480 inatarajiwa
kupitiwa na mwenge wa uhuru katika Wilaya hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizo, Kunambi aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa uhifadhi wa
mazingira na miti asili uliopo katika shehia ya Kitundu.
Miradi mingine ni ya shamba darasa
na bwawa la ufugaji wa samaki, kukagua huduma utoaji wa za afya ya kijiji, kuangalia
darasa la TEHAMA na kituo cha kurekebisha taibia za watumiaji wa dawa za
kulevya (Sober House).
“Maandalizi kwa ajili ya kuupokea mwenge
wa uhuru ndani ya wilaya yetu yanaendelea vyema na ninawaomba wananchi wajitokeze
kwa wingi ili zoezi la kuukimbiza mwenge lifanyike kwa ufanisi mkubwa,”
alieleza Kunambi.
Mwenge wa uhuru ulioanza mbio zake
Mei 17, 2021 katika mkoa wa Kusini Unguja, utaanza mbio zake katika mkoa wa Mjini
Magharibi kupitia wilaya ya Magharibi ‘A’ kuanzia Mei 21, 2021 ambapo utakagua
na kuzindua miradi mbali mbali.
Comments
Post a Comment