Makamu wa Kwanza ataka taasisi za dini zisaidiwe

NA MWANDISHI MAALUM, OMKR

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman, amewahimiza waumini wa dini ya Kiislamu na taasisi mbali mbali nchini kuendelea kuzisaidia taasisi za kidini ili waumini waweze kufanya ibada zao katika mazingira yaliyo bora.

Akizungumza mara baada ya Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Sogea, wilaya ya Mjini Unguja, Alhaj Othman alisema kushiriki katika kutoa misaada ni wajibu wa kila Muislamu, kwani ni kutekeleza maagizo ya Mwenyezi Mungu na hivyo huzidisha imani.

"Waislamu natuweni wenye kujitahidi katika kulitekeleza hili ili tufikie malengo ya kuziimarisha nyumba za Mwenyezi Mungu", alisema Makamu huyo wa Kwanza wa Rais.

Kwa sasa, Msikiti huo wa Sogea, ambao upo katika Wilaya ya Mjini Unguja, umezidiwa na idadi kubwa ya waumini hivyo unahitajika kuvunjwa na kuboreshwa zaidi.

Kwa upande wake, Alhaj Othman aliahidi kushirikiana na waumini hao katika ujenzi wa msikiti wa muda kwa lengo la kuhakikisha wanapata msikiti utakaokuwa na nafasi ya kutosha kwa Waislamu wengi kufanya ibada.

Kwa upande mwengine, Makamu huyo wa Kwanza aliwaambia waumini wenzake kwamba wakati Serikali inaendelea kupambana na uovu nchini, nao wanapaswa kujitahidi katika kuisoma dini ili kuwa na jamii itakayohubiri amani na mshikamano kwa kauli na vitendo.

Mapema, akiwasilisha salamu za waumini kwa serikali, Kiongozi wa Msikiti huo, Sheikh Suleiman Amour, alisema wanawapongeza viongozi wajuu wa serikali kwa kuendeleza umoja na mshikamano.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango