DK. MWINYI ATEMBELEA ENEO LA UWEKEZAJI BANDARI YA  KISASA MANGAPWANI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akisalimiana na baadhi ya viongozi alipowasili katika eneo linalotarajiwa kujengwa kwa bandari ya kisasa Mwangapwani wilaya ya Kaskazibi 'B'.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza CEO wa Kampuni ya United Petroleum Collins Chemngorem (alieshika kipaza sauti). Wa kwanza kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud na kati kati ni Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Rahma Kassim Ali.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Makame Machano Haji akitowa maelezo ya eneo  la Ujenzi wa Bandari ya Kisasa Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini 'B' Unguja wakati wa ziara hiyo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Amour Hamil Bakari, akitoa maelezo ya michoro ya Ramani ya eneo la Ujenzi wa Bandari ya Kisasa katika eneo la Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini 'B' Unguja wakati wa ziara yake kujionea eneo hilo linalotarajiwa ujenzi huo na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutaka ufafanuzi, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud,wakati wa ziara yake kutembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari ya Kisasa katika eneo la Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini 'B' Unguja, akiwa katika eneo la Mradi wa Island Petroleum Group lililojengwa matangi ya mafuta.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar(hawapo pichani) baada ya kumaliza ziara yake kutembelea eneo la ujenzi wa bandari ya kisasa Mwangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.(PICHA ZOTE NA IKULU). 

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango