SIKU YA UHURU WA HABARI DUNIANI

Wadau wataka uhuru zaidi

NA MUHAMMED KHAMIS, TAMWA

WAKATI dunia  ikiadhimisha siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, imelezwa kuwa  ipo haja kwa mamlaka mbali mbali  kutambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari  na uhuru wa kupata habari kwani  ni haki ya kikatiba.

Hayo yamalezwa katika mkutano wa kujadili rasimu ya sheria ya habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) uliopo Maisara mjini Unguja. 

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa habari wanawake TAMWA-Zanzibar, Dk. Mzuri Issa Ali, alisema upatikanaji wa habari unachochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi, hivyo kuna kila sababu wananchi na wanahabri kupewa uhuru wao wa kufanya kazi bila ya kubugudhiwa.

Mkurugenzi huyo aliwataka wanahabari kujikita zaidi katika kujiongezea elimu kwani ndio itakayowasaidia na kuwafanya kuwa wapambanuzi na mambo sambamba na kuepuka changamoto.

Katika hatua nyengine aligusia pia suala la udhalilishaji wa kijinsia kwa wanahabari wanwake visiwani hapa na kusema iwapo kuna wanahabari wanafanyiwa matendo hayo au kuona viashiria wasikae kimya na wanapaswa kutoa taarifa mamlaka husika.

Kwa upande wake mkuu wa kada ya habari Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Imane Osmond Duwe, alisema ipo haja ya wanahabari kufanya kazi zao kwa mujibu wa taaluma na kwa kuwa watafahamu kwa kina nini wanakifanya na wanachokitaka kwa maslahi ya Taifa na jamii kwa ujumla.

Alisema dhana ya uhuru wa habari haishii tu kwa waandishi wa habari bali inakwenda hadi kwa jamii ya kawaida kwa vile jamii nayo inapaswa kupata taarifa juu ya yanayoendelea ndani na nje ya nchi.

Sambamba na hayo alisema alisema kila mtu anapaswa kufahamu kuwa kila aina ya uhuru una mipaka yake hivyo uwepo wa mipaka ya kupata habari isiwe kigenzo cha kuwanyima wanahabari kufanya kazi yao.00000

Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salam kitivo cha sheria Prof.  Chris Maina Peter, alisema wakati dunia inaadhimisha uhuru wakupata habari kila mmoja anapaswa kufahamu kuwa uhuru wa kupata habari ni miongoni mwa haki za msingi kwa kila binadamu.

Alisema kutoka na msingi huo ndio maana serikali zote mbili wakaona umuhimu na kuweka kwenye katiba zao haki ya kupata habari hivyo inapotokea mtu ama taasisi kunyima wengine wasipate habari ni kwenda kinyume na katiba zote mbili.

Maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari hufanyika kila mawaka ifikapo Mei 3  ambapo kwa mwaka huu ujumbe ulikuwa ni 'Habari kwa manufaa ya umma'.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango