Hemed aongoza mazishi marehemu ajali ya basi Shinyanga

NA KASSIM ABDI, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amewaongoza waaumini na wananchi wa Zanzibar katika mazishi Wahda Yussuf, mmoja ya marehemu aliyefariki katika ajali ya basi iliyotokea mkoani Shinyanga usiku wa kumakia Juni 2, mwaka huu.

Hemed alieambatana na viongozi pamoja na watendaji wa serikali, walishiriki katika sala ya maiti iliyosaliwa Masjid Fatma, Kwahani ambapo maziko ya Wahida yalifanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe, wilaya ya Magharibi ‘B’, Unguja.

Makamu wa Pili wa Rais ambae juzi usiku alikuwa miongoni mwa viongozi na wananchi waliopokea miili ya marehemu hao katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, alifanya hivyo kutekeleza ahadi ya serikali iliytoitoa katika Baraza la Wawakilishishi kwamba itasimamia na kugharamia mazishi ya marehemu hao.

Pamoja na wahida, marehemu wengine waliozikwa jana katika maeneo mbali mbali ya Unguja ni Rehema Haji Juma, aliyezikwa katika kijiji cha Kizimkazi na Nassor Juma Khamis aliyekuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Bugema nchini Uganda sawa na Wahida aliyezikwa Bububu, wilaya ya Magharibi ‘A’.

Marehemu hao ni miongoni mwa watu wanne waliofariki katika ajali hiyo ambapo watu 25 walijeruhiwa katika ajali hiyo ambapo Hemed alizitaka familia za marehemu hao kuwa na subra kutokana na msiba waliupata ambao umegusa nyoyo za wananchi wote wa Zanzibar.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango