Simai awataka walimu kutumia huduma za kibenki kujindeleza
NA HAROUB HUSSEIN
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya AmaliZanzibar, Simai Mohammed Said, amewataka
walimu kuzitumia fursa zinazopatikana katika benki ya NMB ili kurahisisha upatikanaji wa mahitaji yao kwa maendeleo ya haraka.
Simai aliyaeleza
hayo wakati akifungua semina ya Siku ya Walimu na NMB iliyofanyika katika
ukumbi wa Michenzani Mall jijini Zanzibar.
Alisema benki ya
NMB ina fursa mbali mbali zinazosaidia wafanyakazi katika mahitaji yao ya kila siku
hivyo ni vyema walimu wakazitumia fursa hizo kujipatia maendeleo ya haraka.
Aidha alisema
katika kujali watumishi wa wizara hiyo benki hiyo imeamua kuweka siku maalum ya
walimu ikiamini walimu ndio msingi mkuu wa maendeleo katika sekta zote.
“Benki hii imeonesha kujali watumishi wetu kwa kuweka siku maalum ya walimu hivyo nakuombeni muwe karibu nayo kwa kuzitumia fursa na huduma zinazopatikana katika benki ya NMB,” alisema Waziri Simai.
Alisema katika
kurahisisha huduma mbali mbali benki hiyo imekua ikitoa huduma hizo kwa njia ya
mtandao wa simu na kufanya huduma zao kupatikana wakati wowote bila ya
usumbufu.
Nae Meneja Mwandamizi wa NMB, Tito Mangesho alisema wamenzisha huduma ya NMB mkononi ambayo itawasaidia walimu katika maendeleo yao ya kila siku, hivyo amewashauri walimu hao kuzitumia ipasavyo fursa zinazopatikana katika benki hiyo kwa maendeleo ya leo na kesho.
Alisema nmb imekua
na fursa mbalimbali ikiwemo ya mikopo ya nyumba kwa nyumba, bima pamoja na
Sanlam life, hivyo aliwashauri walimu kuzitumia fursa hizo na nyenginezo ili
kurahisha maisha yao.
Nae Meneja wa benki
hiyo Kanda ya Zanzibar, Abdalla Duchi alisema benki hiyo ina zaidi ya wateja 2,500,000
nchini kote waliopo katika huduma ya kujihudumia wenyewe jambo lililopunguza misongamano
ya wateja wanaofika ofisini.
Nao baadhi ya washiriki
wa semina hiyo waliishukuru benki ya NMB kwa kuonesha kuwajali na kuwapa fursa
zitakazowakwamua kimaisha.
Walisema mara
nyingi walimu husahauliwa katika masuala mbali mbali ya maendeleo lakini benki
hiyo imeamua kutenga siku maalum kwa walimu ikiwa ni ishara njema kwao ili
waweze kutumia huduma hizo sambamba na kuinua maisha yao.
PICHA:
Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar, Simai Mohamed Said (katikati) akimsikiliza MenejaMwandamini wa huduma za kidigitali kwa wateja wa benki NMB, Tito Mangesho katika mkutano wa siku ya
walimu na NMB kwenye ukumbi wa Michenzani Mall mjini Zanzibar jana.
Comments
Post a Comment