
Kunambi ashukuru mchango wa NMB kuimarisha huduma za jamii NA SHADYA SAID, WMA MKUU wa wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan Peter Kunambi, ameshukuru mchango unaotolewa na sekta binafsi katika maendeleo ya huduma za jamii wilayani humo katika nyanja tofauti. Alieleza hayo wakati akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa mabati 200 na vitanda 30 kwa ajili ya skuli na vituo vya afya wilayani humo kutoka kwa benki ya NMB, hafla iliyofanyika katika skuli ya Msingi Mbuzini. Alisema msaada wa mabati unakwenda kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa katika skuli ya Mbuzini na skuli ya Mtoni Kigomeni kwani baadhi ya madarasa yamekuwa yakihitaji kuezekwa ili kukamilisha ujenzi wa madarasa ulioanza mwaka 2017. “Kuchelewa kukamilika kwa madarasa haya kumesababisha wananfunzi kusoma nje ya madarasa na vitanda hivi vinakwenda kuongeza maeneo ya kupumzikia na kujifungulia katika vituo vyetu vya afya jambo ambalo ni la kushukuriwa sana,” alisema Kunambi. Aidha aliziomb...