NMB yaipa Kusini Unguja msaada wa zaidi ya 25m/-
NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid
ameipongeza benki ya NMB kwa misaada mbali mbali wanayotoa kwa jamii hapa
Zanzibar.
Alisema wananchi wa
maeneo mbali mbali wamekuwa wakilalamikia changamoto za kijamii, ikiwemo sekta
ya elimu kukosekana kwa madarasa ya kusomea baadhi ya madarasa kuvujisha hivyo
misaada iliyotolewa na benki hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondosha
changamoto hizo.
Rashid alieleza
hayo juzi wakati akipokea vifaa vya kuezekea skuli za mkoa huo na vitanda kwa
ajili ya kujifungulia mama wajawazito ili kuwasaidia kwa namna moja ama
nyengine.
Alisema msaada huo
una thamani ya shilingi milioni 25 utatumika kuezekea skuli tatu kwa mkoa huo ikiwemo
ya Kizimkazi, Makunduchi na Binguni.
“Serikali ya
Mapinduzi imekua ikithamini na kutambua misaada inayotolewa na wadau wa
maendeleo kama benki ya NMB kwani imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa kutatua
changamoto za wananchi wetu,” alieleza Mkuu huyo wa amkoa.
Aidha Rashid
aliipongeza benki hiyo kwa kuwa karibu na serikali na kuwasaidia wananchi wa
Zanzibar wakiwemo wakulima wa mwani na wavuvi kwa kuzingatia sera ya Rais wa
Zanzibar kuiendeleza sekta ya uchumi wa buluu.
Katika hafla hiyo
iliyofanyika katika skuli ya Binguni, NMB pia ilikabidhi vitanda 12 kwa ajili
ya vituo vya afya vinavyotoa huduma za
mama na watototo vya sehemu mbali mbali kikiwemo cha Mwera, Chwaka na Unguja
Ukuu.
Aidha aliwaomba
wananchi wa mkoa huo kutumia vyema inayotolewa na benki hiyo kuhusiana na
programu inayojulikana wajibu ambapo inawafahamisha wanafunzi jinsiya kutumie
na watunze fedha.
Rashid aliziomba
taasisi nyengine kuiga mfano wa NMB na kutoa misaada mbali mbali itakayowanufaisha
wananchikutatua changamoto za maji, barabara na masoko ili kukidhi mahitaji ya
wananchi.
Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa
Wateja binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, akizungumza mara
baada ya kukabidhi vifaa hivyo, alisema NMB hiyo imetoa msaada huo kama sehemu
ya utaratibu wa benki hiyo kutenga
asilimia ya faida inayoipata kurejesha kwa wananchi.
Aidha aliahidi kuendelea
kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuimarisha sekta mbali ya
elimu na Afya katika mkoa wa Kusini Unguja ili kuhakikisha wananchi wanafaidika
na huduma hizo.
Akitoa maneno ya shukrani, Awali Mkuu wa wilaya ya Kati, Marina Joel
Thomas, aliishulkuru na kuipongeza NMB kwa kutoa msaada huo, ambapo aliwataka
wasichoke kufanya hivyo ili kukoleza kasi ya maendeleo ya wananchi.
Comments
Post a Comment