HAFLA
YA UZINDUZI WA RASMI MWONGOZO WA MASHAURI KWA MAJAJI NA MAHAKIMU WANAWAKE
KATIKA PICHA
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuzindua rasmi
Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji
wa maamuzi na utendaji haki kwa familia, uliofanyika Oktoba 28, 2021 Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikata
utepe kuzindua rasmi Kitabu cha Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu
Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia.
Uzinduzi huo umefanyika Oktoba, 28 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kushoto
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi, wa pili kushoto Mwakilishi
mkazi wa UN Women hapa nchini bibi. Hodan Addou, kulia Balozi wa Sweden
nchini, Anders Sjoberg na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake
(TAWJA) Jaji Joaquine De Mello.
Baadhi ya wanachama wa chama cha majaji na mahakimu wanawake (TAWJA) na
waalikwa wengine wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakati wa uzinduzi wa mwongozo wa mashauri kwa majaji na
mahakimu wanawake katika utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia, Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Anders Sjoberg mara
baada ya kuzindua rasmi mwongozo wa mashauri kwa majaji na mahakimu wanawake
katika utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia, Ikulu Jijini Dar es
Salaam. (PICHA NA IKULU).
Comments
Post a Comment