Samia awaapisha mawaziri, wajumbe NEC
- LAwataka kuzingatia weledi, uwajibikaji
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewaapisha viongozi mbali mbali aliowateua hivi karibuni na kuwataka kuzingatia weledi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Katika hafla hiyo
iliyofanyika katika ikulu ya Dar es salam, Rais Samia amewaapisha viongozi wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na viongozi walioteuliwa kushika nafasi
katika wizara ya habari na kuwaomba watekeleze majukumu yao kwa ufanisi.
Alisema uteuzi
viongozi hao utaleta uwajibikaji mzuri hasa katika sekta ya habari kwa vile hivi sasa inakwenda
kwenye mabadiko ya kukuza matumizi ya teknologia.
Aidha aliwataka
viongozi hao kuzingatia uwajibikaji na kusimamia utendaji kwenye maeneo yao ya
kazi ili Tanzania ipige hatua za maendeleo kwa kasi zaidi.
Akizungumza wakati
wa hafla hiyo, Makamu wa Rais Dk. Isdori Mpango alisema imeonekana somo la aina
ya uongozi anaoutaka Rais Samia halijaeleweka na Mawaziri na Makatibu wao na
Mkatibu wakuu na Manaibu wake, kwani baadhi yao wanaendeleza mivutana ya
kiutendaji.
Alisema hali hiyo
haipendezi kuendelezwa na kuwaonya viongozi wenye tabia hiyo kuacha mara moja
kwa kuwa Rais alishaonya hatolumbana na mtendaji yoyote ila atatumia kalamu
yake kuchukua maamuzi.
Kutokana na hilo
Makamu Mpango amesema akiwa yeye ndio msaidizi mkuu wa Rais anawaonya watendaji
wenye tabia hiyo kwani hatoachia hali hiyo kuendelea kutokea.
Nae Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa, alimpongeza Rais Samia kwa jitihada zake anazozifanya kwani
kuna miradi mingi anayoitekeleza katika sekta mbali mbali ikiwemo ya michezo
kwani imeonekana kufanya vizuri hivi sasa ndani
na nje ya nchi.
Alisema katika
utekelezaji wa kazi za NEC, serikali haina wasiwasi kwani inafanya kazi kwa
kuzingatia sheria na taratibu ziliopo na kuahidi kuendelea kushirikiana nayo.
Akizungumza Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri, Dk. Tulia Akson, aliwata viongozi wa Tume ya Uchaguzi
kufanya matayarisho ya uchaguzi mapema, badala kusubiri uchaguzi ufike, jambo
ambalo wanasiasa wanatumia kuilalamikia tume ya uchaguzi kutowatendea haki.
Katika hafla hiyo, Rais Samia alimuapisha Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Philipo Gekul kuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo na Mhandishi Kundo Endrea Mathew kuwa Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Jacob Casthom Mwatembela Mwambengele, Magdalena Kamugisha Rwebangira, Asina Abdallah Omar .
Comments
Post a Comment