Kairuki ahimiza biashara kati ya Tanzania, China

NA MWANDISHI WETU

WAFANYABIASHARA wa Tanzania wametakiwa kutumia fursa za uwekezaji nchini china ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi mbili hizo.

Wito huo umetolewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mberwa Kairuki (pichani) mara baada ya ziara ya kutembelea viwanda na kampuni za zinazofanya biashara baina ya nchi mbili hizo hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Tanzania nchini humo ilieleza kuwa Balozi Kairuki amewataka wafanyabiashara hao kufanya hivyo kuunga mkono azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuifungua nchi.

Aidha Balozi Kairuki alieleza kuwa kufanya hivyo pia kutaimarisha mahusiano kati ya mataifa hayo na kuongeza biashara kati yao kama moja ya nyenzo zao.

Katika hatua nyengine Kairuki amewataka watanzania wanaofanya biashara ya bidhaa kutoka nchi hiyo kuhakikisha wanafanya manunuzi ya bidhaa zao kabla ya kuanza kwa maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina yanayoanzia Januari 25, ya kila mwaka.

Alieleza kuwa kuanzia tarehe hiyo, shughuli mbali mbali zikiwemo za biashara husimama kwa muda wa miezi miwili hivyo ni vyema wakafanya mapema manunuzi na mipango ya usafirishaji kabla ya kipindi hicho.

Akizungumzia hali ya biashara na maandalizi ya maonesho ya biashara ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi karibuni, katibu mkuu wa wizara ya biashara na maendeleo ya viwanda, Dk. Islam Seif Salim, alieleza haja ya wafanyabiashara nchini kuingia ubia na wafanyabiashara wa mataifa mengine ili kutanua wigo wa biashara wanazofanya.

Alieleza ili kukuza biashara na kuimarisha uchumi, kuna haja ya wawekezaji wa ndani kuungana na wenzao wa nje kwani kufanya hivyo huongeza utaalamu na kukuza mitaji.

Alisema serikali ya awamu ya nane imeweka mkazo katika sekta ya uwekezaji kwa kutenga maeneo maalum na kuweka vivutio maalum kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Ziara ya Balozi Kairuki katika maeneo hayo kwenye mji wa Guangzhou ilifanyika kwa lengo la kuhamasisha mahusiano ya kibiashara kati ya makampuni ya Tanzania na China.   

 

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango