UZINDUZI WA RIPOTI YA UTAFITI WA VYOMBO VYA HABARI NA URIPOTI WA UCHAGUZI MKUU 2020, DISEMBA 22, 2021 ZANZIBAR

KATIBU Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Suleiman Abdallah Salim (kulia), akikata utepe kuzindua ripoti ya utafiti wa vyombo vya habari na uripoti wa uchaguzi mkuu wa 2020, uliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein uliomo katika jengo la ZURA, Zanzibar.

KATIBU Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Suleiman Abdullah Salim (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa vyombo vya habari na uripoti wa uchaguzi mkuu wa 2020, Dk. Darius Mukiza, wakionesha ripoti hiyo baada ya kuzinduliwa katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein uliomo katika jengo la ZURA, Zanzibar.

Mtafiti Kiongozi, Abadallah Katunzi akitoa maelezo juu ya matokeo ya utafiti vyombo vya habari na uripoti wa uchaguzi mkuu wa 2020 uliofanywa na Shule kuu ya uandishi wa habari ya Chuo Kikuu cha Dar es salam (SJMC) wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo kwa wandishi wa habari na viongozi wa taasisi za habari jijini Zanzibar katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein uliomo katika jengo la ZURA, Zanzibar.


Baadhi ya waandishi wa habari na viongozi wa taasisi za habari walifuatilia uwasilishaji wa ripoti ya utafiti wa vyombo vya habari na uripoti wa uchaguzi mkuu wa 2020 wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein uliomo katika jengo la ZURA, Zanzibar.


MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Dk. Saleh Yussuf Mnemo, akifunga mkutano wa wadau wa habari wa uwasilishaji wa ripoti ya utafiti wa vyombo vya habari na uripoti wa uchaguzi mkuu wa 2020 uliofanywa na Shule kuu ya uandishi wa habari ya Chuo Kikuu cha Dar es salam (SJMC) uliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein uliomo katika jengo la ZURA, Zanzibar.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango