DK. MWINYI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI KWARARA KIDUTANI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, machi 21, 2022 ameweka jiwe la msingi mradi wa uhuishaji na uimarishaji wa mfumo wa usambazaji maji Zanzibar, huko Kwarara Kidutani, ikiwa ni shamrashamra za wiki ya maji duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 22 ya kila mwaka.

Akizungumza katika hafla hiyo alisema upatikanaji wa huduma za maji safi na salama katika maeneo yote ya Zanzibar ni miongoni mwa vipaumbele vya serikali anayoiongoza.

Aidha alisema jitihada zinazochukuliwa na serikali ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2020 - 2025, mipango mikuu ya maendeleo na ahadi alizozitoa wakati wa kampeni.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiondoa kitambaa kuweka jiwe la msingi mradi wa uhuishaji na uimarishaji wa mfumo wa usambazaji maji Zanzibar huko Kwarara Kidutani, wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja. Hafla hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu (ZAWA) Dk. Salha Mohamed Kassim, akitoa maelezo ya ya ujenzi wa matangi ya maji safi na salama Kwarara Kidutani, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa uhuishaji na uimarishaji wa mfumo wa usambazaji maji Zanzibar.

 

BAADHI ya wananchi wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) aliyoitoa wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa uhuishaji na uimarishaji wa mfumo wa usambazaji wa maji Zanzibar.

(PICHA ZOTE NA IKULU ZANZIBAR).

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango