SMZ kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI

NA SABIHA KHAMIS, MAELEZO

WAZIRI wa Afya, Nassor Ahmed Mazrui amesema wizara hiyo inakusudia kuimarisha maabara na kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa sekta ya afya, ili wafikie lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akizungumza na ugeni kutoka Shirika la misaada la Marekani  ofisini kwake Mnazi Mmoja, alisema kuimarisha maabara na kuwapatia mafunzo wafanyakazi kutasaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI.

Alisema wafanyakazi watapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kufanya utafiti ili kuongeza kiwango cha utoaji huduma na kuimarisha sekta ya afya nchini, hasa katika kukabiliana na ugonjwa huo.

“Katika kuwajenga kuimarisha huduma za afya kwa wananchi ni kuwajengea uwezo wafanyakazi wa kufanya utafiti ambao utasaidia kutoa huduma bora kwa jamii”, alisema Mazrui.

Alifahamisha kuwa kupitia shirika hilo wamekuwa mstari wa mbele katika kupambana na UKIMWI nchini, hivyo aliomba kuwepo na ushirikiano  wa  kutosha ili kutokomeza janga hilo.

"Ni kweli hivi sasa tuna waathirika wa UKIMWI 7,600, waathirika 400 kwa mwaka 2020 hadi 2021, hichi si kiwango kidogo katika nchi yetu", alisema waziri huyo.

Mazrui alieleza kuwa wizara hiyo inaendelea na ujenzi wa hospitali 10 za wilaya na moja ya mkoa, ambazo zina malengo ya kuifikishia jamii kupata huduma za afya kwa karibu.

Alifahamisha kuwa katika kupambana na maradhi ya kuambukiza, mke wa Rais wa Zanzibar, mama Maryam Mwinyi yupo mstari wa mbele katika kupambana na kupinga maambukizi ya UKIMWI nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ujumbe huo, Michelle Chevalier alisema lengo la shirika hilo ni kuweka mashirikiano katika mapambano dhidi ya maradhi ya UKIMWI, viashiria vya maradhi hayo na kuwapatia huduma waathirika.

 

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango