Waliojenga viwanja vya serikali kukiona

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Rahma Kassim Ali, amewataka watu waliovamia eneo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar liliopo Tunguu, mkoa wa Kusini Unguja na kujenga kinyume cha sheria, kusimamisha ujenzi huo hadi serikali itakapotoa maamuzi.

Waziri Rahma alitoa agizo hilo hivi karibuni alipofanya ziara ya kutembelea eneo akiambatana na baadhi ya watendaji wa wizara na ofisi ya mkuu wa mkoa kusini Unguja akiwemo mkuu wa mkoa huo, hadid Rashid hadid.

Ziara hizo nio sehemu ya utaratibu aliojiwekea wa kutembelea maeneo ya serikali ambayo baadhi ya wananchi huvamia na kujenga bila ya kua na kibali rasmi cha ujenzi hali inayopelekea kurudisha nyuma. jitihada za kuleta maendeleo nchini.

“Kuna baadhi ya wananchi wanapoona maeneo ya wazi huyavamia na kuanza ujenzi bila ya kutambua kuwa maeneo hayo ni ya serikali hivyo wale wote waliovamia eneo hili, kuanzia leo wasitishe mara moja ujenzi huo na atakaekwenda kinyume na agizo hilo hatua za kisheri zitachukuliwadh yake,” alieleza Waziri huyo.

Aidha Waziri huyo alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa wanapohitaji kufanya ujenzi kwa kufika katika taasisi zinazohusika kupata vibali na klupimiwa maeneo hayo ili kuepusha migogoro ya ardhi inayojitokeza nchini.

"Ili kuepusha migogoro ya ardhi nchini ambayo mengine husababishwa na uvamizi wa maeneo kinyume na utaratibu, niwaombe wananchi wanapotaka kufanya ujenzi kufika katika taasisi husika kwa lengo la kupatiwa utaratibu mzuri wa kisheria," alisema Waziri Rahma.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid, alisema kwa kushirikiana na Ofisi za Mkuu wa Wilaya watahakiksha wanayasimamia  ipasavyo maeneo yote waliyovamia na wananchi ili wasiendelee na ujenzi huo kwa maslahi ya nchi na watu wake.

"Kuna uvamizi mkubwa ambao umefanywa na baadhi ya wananchi ndani ya eneo hili jambo ambalo linasikitisha hivyo nitahakikisha ninalisimamia kwa kuwaita wahusika waliofanya ujenzi na kuwataka kuchukua hatua za kuhama mara moja," alisema Hadid.

Nae Mkurugenzi Upimaji na Ramani kutoka Kamisheni ya ardhi, Juma Ameir, alieleza kusikitishwa kwake na tabia ya baadhi ya wananchi hao kuvamia hadi kiwanja cha mpira ambacho kilishashapimwa na kukabidhiwa taasisi husika.

Ziara ya Waziri Rahma katika maelneo hayo ililenga kuangalia hali halisi ya uvamizi katika maeneo ya ambayo wananchi huvamia kinyume na sheria kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango