Senyamule awaita watanzania kupokea matokeo ya sensa
NA SAIDA ISSA, DODOMA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi katika viwanja vya Jamhuri kushuhudia uzinduzi wa matokeo ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Senyamule wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato Oktoba 30, mwaka huu amesema ni vyema wana-Dodoma na Watanzania kwa ujumla kushiriki katika shughuli hiyo ya kihistoria kufuatia sensa inayofanyika kila baada ya miaka 10.
"Ni
siku ya kipekee na hapa tuna siku moja kufika siku ya kutangaziwa matokeo na
Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, nitoe shime wana Dodoma mje kwa wingi kuanzia saa 12 asubuhi hapa kwenye
viwanja vya Jamhuri,” amueleza Mkuu huyo
wa mkoa.
"Leo (31 Oktoba) kuanzia saa 6 usiku tutakuwa na shamra shamra ya kupiga fataki zikiashiria kuwa Dodoma tupo tayari kuletewa matokeo ya sensa ya watu na makazi hivyo tujitokeze Kwa wingi wana Dodoma" amesema Senyamule
Hata
hivyo uzinduzi wa matokeo hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo "Matokeo ya sensa ya sita 2022, Mipango jumuishi kwa maendeleo
endelevu".
Comments
Post a Comment