Wanahabari watambua mchango wa Senyamule Geita

Na MWANDISHI WETU, DODOMA

CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita (GPC), kimempongeza Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, kwa mabadilko ya utendaji na maendeleo aliyoyafanya alipokua mkuu wa mkoa huo.

Mwenyekiti GPC Renatus Masuguliko ametoa pongezi hizo jana (Disemba 19, 2022) ofisini kwa Mkuu wa mkoa huyo alipofika kwa lengo la kukabidhi hati ya pongezi kwa niaba ya wanachama wa klabu hiyo. 

Masuguliko ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kutambua mchango wa Senyamule alioutoa kwa wananchi wa mkoa wa Geita na chama hicho katika kipindi alichokua Mkuu wa mkoa huo kwa takriban mwaka mmoja kabla ya kuhamishiwa mkoa Dodoma.

Akiambatana na Katibu wa klabu hiyo, Novatus Lyaruu, mwenyekiti Masuguliko amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja ambao Senyamule akiwa mkoani Geita, alifanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika sekta zote na kumpongeza kwa kusimamia kwa vitendo kaulimbiu aliyoianzisha ya ‘Geita ya dhahabu, Utajiri wa heshima’.

“Mheshimiwa Senyamule ulipokuja na hii kaulimbiu mwanzoni hatukukuelewa lakini kwa kipindi kifupi ulifanya mengi katika sekta ya elimu, afya, miundombinu, maji, uchumi na uzalishaji, hivyo watu wa Dodoma mna bahati ya kupata kiongozi mahiri,” amesisitiza Masuguliko mbele ya watendaji wa mkoa na viongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Dodoma (CPC). 

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa mkoa Senyamule ameishukuru GCP na kwa kumpa tunzo hiyo ambayo ni ya heshima kwake na kupongeza mashirikiano aliyoyapayta kutoka kwa makundi mbali mbali mkoani humo.

Ameupongeza uongozi wa chama hicho kwa kuwa mstari wa mbele na wanahabari kwa kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na kusisitiza kuwa kazi hiyo iwe endelevu.

“Ili jamii iweze kunufaika na kufahamu mambo ambayo serikali imekua ikitekeleza katika kuwaletea wananchi maendeleo, nyinyi mlikua mstari wa mbele hivyo naomba muendelee hivyo,” amesema.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma (CPC), Mussa Yusuph aliyeambatana na Katibu wa klabu hiyo, Ben Bago, amemshukuru mkuu huyo wa mkoa kwa kuendelea kushirikiana na wanahabari wa mkoa huo toka alipofika mmkoani humo.

Aidha Mussa alitumia fursa hiyo kumtaarifu Mkuu huyo wa mkoa azma ya Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kuhamishia Makao Makuu yake mkoani Dodoma kutoka Mwanza na kumuhakikishia mkuu huyo wa mkoa ushirikiano wa wanahabari wa mkoa huo.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule (katikati) akiwa katika picha na viongozi wa GPC na CPC baada ya kupokea hati ya pongezi ya kutambua mchango wake alipoua Mkuu wa mkoa wa Geita. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa GPC Renatus Masuguliko, Mwenyekiti wa CPC Mussa Yusuph, Katibu wa GPC Novatus Lyaruu na Katibu wa CPC, Ben Bago.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango