TANESCO yazindua programu kukuza usawa kijinsia

NA SAIDA ISSA, DODOMA NA SAIDA ISSA, DODOMA SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limezindua programu ya miaka minne ya mpango wa kuimarisha usawa wa jinsia wenye lengo la kutatua changamoto za wanawake katika maeneo ya kazi ikiwemo ya vitendo vya unyanyasaji. Akizugumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato, alisema mradi huo unalenga kutengeneza sera za shirika na kujenga uwezo kuhusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia. Alisema mradi huo, utasaidia kuwepo kwa taarifa sahihi za unyanyasaji wa kijinsia katika shirika, kuruhusu fursa ya ukuzaji taaluma kwa wafanyakazi wanawake na kuongeza mafunzo kwa vitendo kwa wafanyakazi wanawake waliopo kazini. Alieleza kuwa mradi huu unatekelezwa na TANESCO lengo ni kuhakikisha watumishi wanaofanya kazi katika taasisi hiyo wanapata haki sawa, lengo ni kuhakikisha nafasi zinazojitokeza zinahusisha jinsia zote bila ubaguzi na kujenga usawa. "Katika...