Masheha, Madiwani wapewa elimu miradi ya TASAF
NA MWANDISHI WETU, PEMBA
Ofisa
Mdhamini Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Pemba, Abdullwahab
Said Bakari, alitoa wito huo na kusema kufanya hivyo ni kutekeleza malengo ya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar (SMZ) ya kupunguza umaskini kwa wananchi na kuongeza kasi ya ukuaji wa
uchumi.
Alisema serikali imepanga mpango wa kupunguza umaskini na kuongeza ukuaji wa uchumi jumuishi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) ambayo imeweka sifa kwa walengwa wake.
Bakari alieleza hayo wakati
akifungua mafunzo kwa Masheha na Madiwani wa mkoa wa Kusini Pemba yaliyolenga
kuwajengea uwezo viongozi wanaosimamia shughuli za mpango wa kunusuru kaya
maskini Tanzania, ulioandaliwa na TASAF Pemba.
“Hivi sasa kuna changamoto nyingi nyinyi kutoka kwa walengwa, Masheha na Madiwani mnatakiwa kuwa mabalozi, pia wasemaji wazuri wa kuisema TASAF kwa jamii”, alisema.
Aidha alisema changamoto kubwa
zifikishwa kwa watendaji ili kupatiwa ufumbuzi, yale maneno ambao sio sahihi
yataweza kupatiwa ufafanuzi, ili changamoto zinazotokezea za wananchi
zinahitaji kutatuliwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF Tanzania, Mkurugeni Uratibu, Haika Shayo, alisema mafunzo
hayo yatasaidia kufanikisha lengo la mpango, kwani kutakuwa ni mwanzo mzuri kwa
viongozi hao kufahamu kikamilifu juu ya masuala na shughuli mbali mbali za
TASAF.
Aidha aliwataka walengwa kuhakikisha wanafungua akaunti benki kwa ajili ya kupokelea fedha zao, kwani suala la fedha mkononi limeshaondoka,” alisema.
Naye Ofisa ufuatiliaji TASAF Pemba,
Abrahman Khamis, alisema madhumuni ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi
wanaosimamia shughuli za mpango, kuwa na uelewa wakutosha juu ya taratibu
zinazotumika kusimamia na kufuatilia shuhuli za mpango.
Aidha Mratibu wa TASAF Pemba, Mussa
Said, alisema lengo ni kuongeza kipato kwa wananchi, pamoja na kuongeza ujuzi
kupitia miradi wanayoianzisha kwenye shehia zao, kwani ushirikishwaji wananchi
ni jambo kubwa katika kuibua miradi ya maendeleo kupitia walengwa wa mpango wa
kunusuru kaya masikini.
Hata hivyo, kwa upande wa Masheha
waliahidi kwenda kusimamia kikamilifu, shughuli zote za TASAF zinazofika katika shehia zao, kwani wao ndio
viongozi wa serikali kwenye ngazi nya
shehia.
Comments
Post a Comment