Ibueni mbinu zitakazowavutia wafadhili - Simbaya

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Keneth Simbaya (pichani kushoto), ameushauri uongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kubuni mbinu zitakazoimarisha utendaji na kujitegemea.


Simbaya aliyekuwa Zanzibar kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari (WPFD) iliyoadhimishwa kitaifa mjini Zanzibar, alifanya ziara katika ofisi za klabu hiyo Kijangwani na kukutana na viongozi na badhi ya wananchama.

Aidha ameeleza kuridhwa na mipango ya Klabu hiyo na kuwataka kuondokana na utegemezi wa mfadili mmoja badala yake kuwa na mikakati itakayowasaidia wanachama wa klabu hiyo kupata maendeleo.

Aidha alieleza kuwa muelekeo wa UTPC ni kuzijengea uwezo klabu na viongozi wake ili ziweze kujisimamia kama njia moja ya kuuimarisha muungano huo unaounndwa na vilabu 28 vya waandishi wa habari vya Tanzania bara na Zanzibar.

"Lazima mtafute mbinu za kufikia ndoto zenu kama viongozi kukidhi matarajio ya wanachama wenu kama mlivyoeleza na hili litawezekana kwa kutumia zaidi ya mfadhili mmoja", amesema Simbaya.

Baadhi ya viogozi na wanachama wa ZPC wakiwa kikaoni

Awali Katibu Mkuu wa klabu hiyo Mwinyimvua Nzukwi, alieleza kuwa wamejipanga kujenga uwezo wa wanachama wake ili kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia lakini pia mabadiliko ya sheria ya habari yanayotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.


"Kuna mambo mengi ya maendeleo ya klabu na wananchama wake tunayoyatarajia lakini kubwa kwa sasa ni kutafuta mbinu za kuwasaidia wanachama wetu wenye viwango vidogo vya elimu ili wasijekutolewa na marekebisho ya sheria au ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano", amesema.

Nae mwenyekiti wa klabu hiyo, Abdallah Mfaume ambaye pia ni Mjumbe wa bodi ya UTPC, alimpongeza Mkurugenzi huyo kwa kuamua kufanya ziara hiyo jambo lililotoa nafasi ya kubadilishana mawao na uzoefu utakaosaidia kuiimarisha ZPC na UTPC.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango