Puma Energy, KIST zasaini makubaliano kukuza ujuzi

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania imesani makubaliano ya utekelezaji wa programu ya kukuza ujuzi kwa wahitimu wa Taasisi ya Teknolojia Karume (KIST) na Pamoja Zanzibar.

Akizindua programu hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Muhamed Mussa, amewataka wahitimu waliopata fursa ya kufanya kazi katka kampuni ya  kuitumia vyema ili kukuza ujuzi na uwezo wao katika kazi.

Alitoa wito huo jana wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya progrmu ya kuendeleza ujuzi wa wahitimu wa Taaasisi ya Teknolojia Karume (KIST) na taasisi ya Pamoja Zanzibar kwa upande mmoja na kampuni ya Puma Energy Tanzania iliyofanyika Mbweni mjini unguja.

Alieleza kuwa kutokana na mifumo ya elimu na ujuzi iliyopo nchni inazingatia wanafunzi kusoma ili kufaulu mitihani, hivyo mpango huo utawasaidia wahitimu hao kupata ujuzi na uzoefu utakaoimarisha maarifa waliyoyapata chuoni.

Lela aliishukuru kampuni ya Puma kwa kuingia makubaliano hayo na taasisi mbili hizo hatua itakayotoa nafasi za ajira kwa vijana wa Zanzibar lkn pia kuimarisha huduma katika maeneo mbali mbali.

Aidha aliwahakikishia wabia katika utekelezaji wa makubaliano hayo kwamba serikali itatoa kila aina ya ushirikiano kufanikisha utekelezajj wa makubaliano hayo.

Nae Afisa Mwendeshajii Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Afrika, Hassan ben Ouattara, alieleza kuwa kampuni hiyo itaendelea kuwekeza Zanzibar ili kuimarisha huduma zinazotolewa n kampiuni hiyo kwa mashirika mbali mbali ya ndege katika viwanja vya ndege vya hapa nchini.

Alieleza kuwa programu ya wahitimu wa taasisi hiyo ni miongoni mwa mipango ya kampuni ya Puma kuimarisha ujuzi na upatikanaji wa ajira kwa vijana wa Tanzania hivyo aliwakaribisha vijana na kuwataka kufanya kazi kwa bidii.

“Sisi (Puma Energy Africa) tumekua na programu nyingi zinazolenga kukuza ujuzi, kazi na utaalamu kwa vijana tukiamini kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaendeleza ukombozi wa bara la afrika na watu wake”, alieleza Outtara.

Akizungumzia programu hiyo, Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah, alieleza kuwa ushirikiano huo ni sehemu ya dhamira ya kampuni hiyo kuwajibika kwa jamii ya Zanzibar.

Alieleza kuwa kupitia mpango huo, wahitimu wa hao watajifunza kuhusu uendeshaji na utendaji wa kila siku wa bohari za kampuni hiyo na shughuli za matengenezo katika kituo cha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA) Zanzibar.

“Kama sehemu ya ratiba ya mafunzo, washiriki wa KIST watajifunza kuhusu uendeshaji na utendaji wa bohari zetu na shughuli za matengenezo na wahitimu wa Pamoja Znzibar watajifunza kuhusu matengenezo ya magari”, alieleza Fatma.

Nae Mkurugenzi wa KIST Dk. Mamoud abdulwahid alawi, alieleza kuwa programu hiyo inatoa fursa kwa wahitimu wa taasisi hiyo kutumia ujuzi walioupata chuoni katika mazingira ya kazi.

“Mpango huu umeanzishwa kwa umakini mkubwa ili kuwafundisha wahitimu watano ujuzi watakaouhitaji ili kuhimili mazingira ya kazi na unatoa mwanya w kuajiriwa kwa muda mrefu na kampuni hii ambayo ni kiini cha uchumi wa Zanzibar”, alieleza Dk. Alawi.

Mmoja ya wahitimu watano waliopata fursa hiyo Ghulam Abdallah, alieleza kuwa ameurahishwa na mpango huo ambao utamsaidia kutumia vyema ujuzi alioupata chuoni.

“Nimefurahi kuwa miongoni mwa wahitimu waliochaguliwa kushiuriki programu hii kwani nmejifunza mengi kwa nadharia lakini sasa ninaenda kupata fursa ya kuongeza ujuzi na kupata uzoefu”, alieleza Ghullam.

Programu hiyo itakayotekelezwa kwa pamoja kati ya KIST, Pamoja Zanzibar na kampuni ya Puma, itaendeshwa kwa miaka mitatu kwa wahitimu watano kufanya kazi katika kampuni hiyo na kuelezwa kuwa inaweza kupanuliwa ili kuongeza idadi ya washiriki na fani nyengine za ufundi mali na ufundi magari waliyotoka wahitimu hao.

Comments

Popular posts from this blog

ZALIRI, FLI zaingia makubaliano kuimariusha sekta mifugo

Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya

Uislam unakubali uzazi wa mpango