Dk. Mwinyi aeleza dhamira CCM kufanya vikao vikuu Z'bar
NA MWANDISHI WETU
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuwa chama hicho kitafanya mkutano mkuu wake taifa ndani ya visiwa vya Zanzibar ilimkutoa fursa kwa wajumbe kushuhudia maendeleo yaliyopatikana.
Dk. Mwinyi ambaye pia
ni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyasema hayo
Ikulu Zanzibar alipokua akizungumza na Wenyeviti wa mikoa wa chama hicho kutoka
mikoa yote ya Tanzania waliofika kumsalimia.
Alisema CCM Zanzibar,
itahakikisha inalifanikisha azma hiyo na kuwezesha uptikanaji wa rasilimali
zote ikiwemo eneo muafaka la kuhudumia wajumbe wote wa mkutano huo na mikutano
mengine ya Halmashauri Kuu taifa ikiwa ni pamoja na kujenga ukumbi mkubwa wa
mikutano.
Alieleza kuwa uwepo
wa ukumbi huo utaiwezesha nchi nzima kuwa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya utekelezaji
wa Ilani ya chama hicho.
Aidha Dk. Mwinyi, alimpongeza Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassa kwa kuwaalika viongozi hao wa chama kuhudhuria Tamasha la Kizimkazi lililoanza siku chache zilizopita.
Katika hatua
nyengine, Dk. Mwinyi alisifu uamuzi wa viongozi hao kutembelea Zanzibar kwani ni
moja ya njia ya kukuza na kudumisha ushirikiano, umoja na mshikamano ndani ya
chama, hivyo aliwaomba viongozi hao kutembelea maeneo mengine na kujionea
miradi ya maendeleo ya chama hicho kwa kubadilishana uzoefu.
Akizungumza Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, Talib Ali Talib, alimueleza Makamu Mwenyekiti
huyo jinsi walivyoupokea ugeni huo na kuutembeza maeneo mbali mbali ya historia
ya Zanzibar ikiwemo Mji Mkongwe wa Zanzibar na kuangalia maeneo mengine ya
Utalii.
Naye, Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Tabora, Hassan Wakasuvi. Akizungumza kwa niaba ya Wenyeviti wenzake
alimpongeza Dk. Mwinyi kwa hatua kubwa za maendeleo aliyoifanikisha ndani ya
kipindi kifupi cha uongozi wake.
Aidha kupitia dk. Mwinyi,
Wenyeviti hao walimshukuru Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mwaliko aliowapa kuhudhuria Tamasha la
Kizimkazi na kujionea mandhari halisi ya Zanzibar kwa waliokuwa hawajawahi
kufika.
Aidha walisifu hatua
hiyo na kuitaja kuwa ni njia ya kukuza utalii wa ndani na kudumisha ushirikiano
baina ya viongozi wa chama hicho wa mikoa ya Tanzania bara na zanzibar.
Comments
Post a Comment