Ibueni changamoto zinazokamisha usawa wa kijinsia - Simbaya
NA MWANAISHA SHARIA, MOROGORO
Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya alipokua akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za usawa wa kijinsia yaliyofanyika hoteli ya Flomi, mjini Morogoro.
Amesema wandishi wa habari wana nguvu ya kufikisha ujumbe kwa jamii hivyo wana jukumu la kuhakikisha wanatoa elimu ya usawa wa kijinsia ili kutatua changamoto zilizopo.
"Waandishi wa habari mtakapoibua kero za wanawake na kuzisemea mtaleta mabadiliko kwa wanawake hao lakini pia jamii nzima kwani kupitia kwao ukatili na ukandamizaji wanawake na watoto wa kike utaondoka”, alieleza Simbaya.
Aidha Mkurugenzi huyo
amewataka waandishi waliopatiwa mafunzo hayo kutumia vizuri elimu hiyo kwa kuandika
habari na kuanda vipindi kuhusu usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko katika
jamii.
Nae Afisa Miradi
anayesimamia masuala ya jinsia UTPC, Hilda Kileo, amesema lengo la mafunzo hayo
ni kuwaongezea ujuzi wandishi wa habari kuandika habari kuhusu usawa wa
kijinsia na uwezeshaji wanawake katika nyanja za uchumi, siasa na jamii.
Akiwasilisha mada katika
mafunzo hayo, Mkufunzi Deo Tembo, amesema endapo kutakua na usawa wa kijinsia
na ushirikishwaji wa wanawake katika mambo mbali mbali kutaongeza Fursa za
ukuaji wa uchumi na maendeleo.
Nao baadhi ya washiriki
wa mafunzo hayo Mgongo Kaitika na Zaituni Juma wameushukuru uongozi wa UTPC kwa
kutoa mafunzo waliyowapatika na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuleta mabadiliko
katika jamii.
Mafunzo hayo ya siku
mbili yanayohusisha waandishi wa habari 28 wanachama wa klabu za waandishi wa habari
za Tanzania bara na Zanzibar yameandaliwa na UTPC ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa mpango mkakati wake unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la
watu wa Sweden (SIDA).
Comments
Post a Comment